Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake, na kuyafungia katika giza nene,

  2. nilipoamuru mipaka yake, na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,

  3. ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu, na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano?

  4. Ni nani ampaye kunguru chakula wakati makinda yake yanamlilia Mungu, yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?

  5. Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake, nchi ya chumvi kuwa makao yake.

  6. kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima, wala hakumpa fungu la akili njema.

  7. Bwana akamwambia Ayubu:

  8. “Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”

  9. Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:

  10. “Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.

  11. Ndipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli:

  12. “Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.

  13. “Je, utabatilisha hukumu yangu? Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe?

  14. Je, una mkono kama wa Mungu, nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?

  15. Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.

  16. “Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi, niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe, anayekula majani kama ngʼombe.

  17. Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu, lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.

  18. Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza. Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu?

  19. Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.

  20. “Sitashindwa kunena juu ya maungo yake, nguvu zake na umbo lake zuri.

  21. Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:

  22. “Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.

  23. “Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena; nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’

  24. Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako, lakini sasa macho yangu yamekuona.

  25. Baada ya Bwana kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.