Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.”

  2. Kwa hiyo Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi wakafanya kama Bwana alivyowaambia; naye Bwana akayakubali maombi ya Ayubu.

  3. Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, Bwana akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni.

  4. Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote Bwana aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.

  5. Bwana akaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, ngamia elfu sita, jozi za mafahali elfu moja, na punda wa kike elfu moja.

  6. Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.

  7. Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia.

  8. Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

  9. Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.

  10. Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,

  11. “Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”

  12. Nitatangaza amri ya Bwana: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa.

  13. Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako.

  14. Utawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”

  15. Mtumikieni Bwana kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka.

  16. Zaburi ya Daudi. Alipomkimbia mwanawe Absalomu. Ee Bwana, tazama adui zangu walivyo wengi! Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!

  17. Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.”

  18. Lakini wewe, Ee Bwana, ni ngao pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.

  19. Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.

  20. Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.

  21. Ee Bwana, amka! Niokoe, Ee Mungu wangu! Wapige adui zangu wote kwenye taya, vunja meno ya waovu.

  22. Kwa maana wokovu watoka kwa Bwana. Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

  23. Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi. Nijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Nipumzishe katika shida zangu; nirehemu, usikie ombi langu.

  24. Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu kuwa aibu mpaka lini? Mtapenda udanganyifu na kufuata miungu ya uongo mpaka lini?

  25. Fahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga wale wamchao kwa ajili yake; Bwana atanisikia nimwitapo.