God
Mistari inayomtaja God
Bwana na awahukumu kabila za watu. Nihukumu Ee Bwana, kwa kadiri ya haki yangu, kwa kadiri ya uadilifu wangu, Ewe Uliye Juu Sana.
Ee Mungu mwenye haki, uchunguzaye mawazo na mioyo, komesha ghasia za waovu na ufanye wenye haki waishi kwa amani.
Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana, awaokoaye wanyofu wa moyo.
Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu aghadhibikaye kila siku.
Kama hakutuhurumia, atanoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake.
Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto.
Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana.
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu.
Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa, kwa sababu ya watesi wako, kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi.
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha,
mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali?
Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji ya utukufu na heshima.
Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.
Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa muth-labeni. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.
Nitafurahi na kushangilia ndani yako. Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.
Adui zangu wamerudi nyuma, wamejikwaa na kuangamia mbele zako.
Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; umeketi kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki.
Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu; umeyafuta majina yao milele na milele.
Bwana anatawala milele, ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.
Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki, atatawala mataifa kwa haki.
Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida.
Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe Bwana, hujawaacha kamwe wakutafutao.
Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni, tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.
Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka, hapuuzi kilio cha wanaoonewa.