Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Tribes of Israel

241 mistari · 21 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Upande wa kaskazini kutakuwa na makundi ya kambi ya Dani, chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.

  2. Kundi lake lina watu 62,700.

  3. Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani.

  4. Kundi lake lina watu 41,500.

  5. Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.

  6. Kundi lake lina watu 53,400.

  7. Wanaume wote walio katika kambi ya Dani ni 157,600. Wao watakuwa wa mwisho kuondoka chini ya alama yao.

  8. Hawa ndio Waisraeli, wakiwa wamehesabiwa kufuatana na jamaa zao. Wote walio kambini kwa makundi yao ni watu 603,550.

  9. Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya alama yao. Nashoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao.

  10. Nethaneli mwana wa Suari alikuwa kiongozi wa kabila la Isakari,

  11. naye Eliabu mwana wa Heloni alikuwa kiongozi wa kabila la Zabuloni.

  12. Ndipo Maskani iliposhushwa, nao wana wa Gershoni na wana wa Merari ambao waliibeba wakaondoka.

  13. Vikosi vya kambi ya Reubeni vilifuata, chini ya alama yao. Elisuri mwana wa Shedeuri alikuwa kiongozi wao.

  14. Shelumieli mwana wa Surishadai aliongoza kikosi cha kabila la Simeoni,

  15. naye Eliasafu mwana wa Deueli aliongoza kikosi cha kabila la Gadi.

  16. Kisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilikuwa isimamishwe kabla wao hawajafika.

  17. Vikosi vya kambi ya Efraimu vilifuata, chini ya alama yao. Elishama mwana wa Amihudi alikuwa kiongozi wao.

  18. Gamalieli mwana wa Pedasuri aliongoza kikosi cha kabila la Manase,

  19. naye Abidani mwana wa Gideoni alikuwa kiongozi wa kikosi cha kabila la Benyamini.

  20. Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao.

  21. Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri,

  22. naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali.

  23. Huu ndio ulikuwa utaratibu wa kuondoka wa vikosi vya Waisraeli walipokuwa wanaondoka.

  24. Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa: kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki; kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;

  25. kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.