Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Tribes of Israel: Divided into families

48 mistari · 21 vipengele

Mistari kuhusu Divided into families

Chuja kwa kitabu
  1. “Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja.

  2. Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa: kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki; kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;

  3. kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.

  4. Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.

  5. Mwana wa Palu alikuwa Eliabu,

  6. nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Mose na Aroni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi Bwana.

  7. Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo.

  8. Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.

  9. Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli; kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini; kutoka wa Yakini, ukoo wa Wayakini;

  10. kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera; kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli.

  11. Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200.

  12. Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni; kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi; kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;

  13. kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni; kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri;

  14. kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi; kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli.

  15. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.

  16. Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.

  17. Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela; kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi; kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera.

  18. Wazao wa Peresi walikuwa: kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni; kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.

  19. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500.

  20. Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola; kutoka kwa Puva, ukoo wa Wapuva;

  21. kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu; kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.

  22. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300.

  23. Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi; kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni; kutoka kwa Yaleeli, ukoo wa Wayaleeli.

  24. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500.

  25. Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa: