Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu The Levites

255 mistari · 63 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wazao wa Gershoni: Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi, Yahathi akamzaa Zima,

  2. Zima akamzaa Yoa, Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera, Zera akamzaa Yeatherai.

  3. Wazao wa Kohathi: Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora, Kora akamzaa Asiri,

  4. Asiri akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,

  5. Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli, Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli.

  6. Wazao wa Elikana walikuwa: Amasai na Ahimothi,

  7. Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai, Sofai akamzaa Nahathi,

  8. Nahathi akamzaa Eliabu, Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Samweli.

  9. Wana wa Samweli walikuwa: Yoeli mzaliwa wake wa kwanza, na Abiya mwanawe wa pili.

  10. Wafuatao ndio wazao wa Merari: Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni, Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,

  11. Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaya.

  12. Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko.

  13. Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

  14. Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao: Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa: Hemani, mpiga kinanda, alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,

  15. mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa,

  16. mwana wa Sufu, mwana wa Elikana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,

  17. mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,

  18. mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,

  19. mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;

  20. na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume: Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,

  21. mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya,

  22. mwana wa Ethni, mwana wa Zera, mwana wa Adaya,

  23. mwana wa Ethani, mwana wa Zima, mwana wa Shimei,

  24. mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.

  25. Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto: Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki,