Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu The Levites

255 mistari · 63 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,

  2. mwana wa Amsi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri,

  3. mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.

  4. Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu.

  5. Mabawabu katika Hekalu la Bwana waliorudi walikuwa: Shalumu, Akubu, Talmoni, Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mlinzi wao mkuu.

  6. Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi.

  7. Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya Bwana.

  8. Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, naye Bwana alikuwa pamoja naye:

  9. Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania.

  10. Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli.

  11. Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba ya Bwana, nyumba iliyoitwa Hema.

  12. Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini.

  13. Ndugu zao katika vijiji vyao walikuwa wakija mara kwa mara na kuwasaidia katika kazi zao kwa vipindi mbalimbali vya siku saba.

  14. Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu.

  15. Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi:

  16. Kutoka wazao wa Kohathi, Urieli kiongozi na ndugu zake 120,

  17. Kutoka wazao wa Merari, Asaya kiongozi na ndugu zake 220.

  18. Kutoka wazao wa Gershoni, Yoeli kiongozi na ndugu zake 130.

  19. Kutoka wazao wa Elisafani, Shemaya kiongozi na ndugu zake 200.

  20. Kutoka wazao wa Hebroni, Elieli kiongozi na ndugu zake 80.

  21. Kutoka wazao wa Uzieli, Aminadabu kiongozi na ndugu zake 112.

  22. Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.

  23. Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000.

  24. Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la Bwana na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi,

  25. na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu Bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”