Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Select Readings

802 mistari · 47 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu, na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao:

  2. ili kuonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka Agano lake takatifu,

  3. kiapo alichomwapia baba yetu Abrahamu:

  4. kutuokoa kutoka mikononi mwa adui zetu, tupate kumtumikia yeye pasipo hofu

  5. katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote.

  6. “Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana; kwa kuwa utamtangulia Bwana na kuandaa njia kwa ajili yake,

  7. kuwajulisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao,

  8. kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu, nuru itokayo juu itatuzukia

  9. ili kuwaangazia wale waishio gizani na katika uvuli wa mauti, kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”

  10. Yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu katika roho; akaishi nyikani hadi siku ile alipojionyesha hadharani kwa Waisraeli.

  11. Wakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Yesu, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

  12. Yesu akamjibu, “Imeandikwaje katika Sheria? Kwani unasoma nini humo?”

  13. Akajibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”

  14. Yesu akamwambia, “Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi.”

  15. Lakini yule mtaalamu wa sheria, akitaka kujionyesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Yesu, “Jirani yangu ni nani?”

  16. Yesu akamjibu akasema, “Mtu mmoja alikuwa akiteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, naye akaangukia mikononi mwa wanyangʼanyi. Wakampiga, wakaondoka, wakamwacha akiwa karibu kufa.

  17. Kuhani mmoja alikuwa akipitia njia ile, alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani.

  18. Vivyo hivyo, Mlawi mmoja naye alipofika mahali pale, alimwona, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani

  19. Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri alipomwona, alimhurumia.

  20. Akaenda alipokuwa na akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, kisha akayafunga. Ndipo akampandisha kwenye punda wake, akampeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni na kumtunza.

  21. Kesho yake, yule Msamaria akachukua dinari mbiliakampa yule mwenye nyumba ya wageni na kusema, ‘Mtunze, nami nirudipo nitakulipa gharama yoyote ya ziada uliyotumia kwa ajili yake.’

  22. “Ni yupi basi miongoni mwa hawa watatu wewe unadhani ni jirani yake yule mtu aliyeangukia mikononi mwa wanyangʼanyi?”

  23. Yule mtaalamu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemhurumia.” Ndipo Yesu akamwambia, “Nenda, ukafanye vivyo hivyo.”

  24. Yesu akaendelea kusema: “Kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na wana wawili.

  25. Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Hivyo akawagawia wanawe mali yake.