Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Salvation

158 mistari · 106 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kinywa changu kitasimulia haki yako, wokovu wako mchana kutwa, ingawa sifahamu kipimo chake.

  2. Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana, utupe wokovu wako.

  3. Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu.

  4. Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

  5. Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, uwe msaada wangu unapowaokoa,

  6. Nimrudishie Bwana nini kwa wema wake wote alionitendea?

  7. Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la Bwana.

  8. Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako,

  9. Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.

  10. Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli.

  11. Wokovu uko mbali na waovu, kwa kuwa hawatafuti maagizo yako.

  12. Ee Bwana, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu.

  13. Nitawavika makuhani wake wokovu, nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha.

  14. Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.

  15. Hakika Mungu ni wokovu wangu; nitamtumaini wala sitaogopa. Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu.”

  16. Kwa furaha mtachota maji kutoka visima vya wokovu.

  17. Katika siku ile watasema, “Hakika huyu ndiye Mungu wetu; tulimtumaini, naye akatuokoa. Huyu ndiye Bwana, tuliyemtumaini; sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.”

  18. Katika siku ile, wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda: Tuna mji ulio na nguvu, Mungu huufanya wokovu kuwa kuta zake na maboma yake.

  19. waambieni wale wenye mioyo ya hofu, “Kuweni hodari, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja, pamoja na malipo ya Mungu, atakuja na kuwaokoa ninyi.”

  20. Lakini Israeli ataokolewa na Bwana kwa wokovu wa milele; kamwe hutaaibika wala kutatahayarika, milele yote.

  21. “Kusanyikeni pamoja mje, enyi wakimbizi kutoka mataifa. Wale wabebao sanamu za mti ni watu wasio na akili, wale waombao miungu isiyoweza kuokoa.

  22. Tangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo, wao na wafanye shauri pamoja. Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani, aliyetangaza tangu zamani za kale? Je, haikuwa Mimi, Bwana? Wala hapana Mungu mwingine zaidi yangu mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hapana mwingine ila mimi.

  23. “Nigeukieni mimi, nanyi mkaokolewe, enyi miisho yote ya dunia; kwa maana mimi ndimi Mungu, wala hapana mwingine.

  24. yeye asema: “Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kurejeza makabila ya Yakobo, na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi? Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa, ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.”

  25. Hili ndilo asemalo Bwana: “Wakati wangu uliokubalika nitakujibu, nami katika siku ya wokovu nitakusaidia; nitakuhifadhi, nami nitakufanya kuwa agano kwa ajili ya watu, ili kurudisha nchi na kugawanyia urithi tena wale waliokuwa ukiwa,