Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Consolation Under Affliction

87 mistari · 22 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mungu wa milele ni kimbilio lako, na chini kuna mikono ya milele. Atamfukuza adui yako mbele yako, akisema, ‘Mwangamize yeye!’

  2. Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai, naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.

  3. Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu;

  4. Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima.

  5. Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji.

  6. Hata kama baba yangu na mama wakiniacha, Bwana atanipokea.

  7. Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.

  8. Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na chochote.

  9. Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu chochote kilicho chema.

  10. Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, atamwinua kutoka kitandani mwake.

  11. Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini, yule aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake.

  12. Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie, ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi.

  13. Najua kwamba wapendezwa nami, kwa kuwa adui yangu hanishindi.

  14. Katika uadilifu wangu unanitegemeza na kuniweka kwenye uwepo wako milele.

  15. Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, Mwokozi wangu na

  16. Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.

  17. Dharau zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, wa kunituliza, lakini sikumpata.

  18. Usinitupe wakati wa uzee, wala usiniache nguvu zangu zinapopungua.

  19. Ee Mungu, usiniache, hata niwapo mzee wa mvi, mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho, nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye.

  20. Utaongeza heshima yangu na kunifariji tena.

  21. Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu, faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.

  22. Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.

  23. Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.

  24. Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifajiri lini?”

  25. Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua: Nikaona machozi ya walioonewa, wala hawana wa kuwafariji; uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowaonea, wala hawana wa kuwafariji.