Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kumbukumbu 22:10takriban 1451 KK

    Usilime kwa maksai aliyefungwa nira pamoja na punda.

  2. Kumbukumbu 22:11takriban 1451 KK

    Usivae nguo za sufu na kitani zilizofumwa pamoja.

  3. Kumbukumbu 22:12takriban 1451 KK

    Fanya vishada kwenye pembe nne za joho unalovaa.

  4. Kumbukumbu 22:13takriban 1451 KK

    Ikiwa mtu atamwoa mke na, baada ya kufanya naye tendo la ndoa, akamchukia,

  5. Kumbukumbu 22:14takriban 1451 KK

    akimsingizia na kumwita jina baya, akisema, “Nilimwoa mwanamke huyu, lakini nilipomkaribia sikupata uthibitisho wa ubikira wake”

  6. Kumbukumbu 22:15takriban 1451 KK

    ndipo baba na mama wa msichana wataleta uthibitisho kwamba alikuwa bikira kwa wazee wa mji kwenye lango.

  7. Kumbukumbu 22:16takriban 1451 KK

    Baba wa msichana atawaambia wazee, “Nilimwoza binti yangu kwa huyu mwanaume, lakini hampendi.

  8. Kumbukumbu 22:17takriban 1451 KK

    Sasa amemsingizia na kusema, ‘Sikumkuta huyu binti akiwa bikira.’ Lakini hapa kuna uthibitisho wa ubikira wa binti yangu.” Kisha wazazi wake wataonyesha nguo zake kwa wazee wa mji,

  9. Kumbukumbu 22:18takriban 1451 KK

    nao wazee watamchukua huyo mwanaume na kumwadhibu.

  10. Kumbukumbu 22:19takriban 1451 KK

    Watamtoza shekeli mia moja za fedha na kupewa wazazi wa msichana, kwa sababu mwanaume huyu amempa bikira wa Kiisraeli jina baya. Ataendelea kuwa mke wake; kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

  11. Kumbukumbu 22:20takriban 1451 KK

    Hata hivyo, kama shtaka ni la kweli na hakuna uthibitisho juu ya ubikira wa huyo msichana ulioweza kupatikana,

  12. Kumbukumbu 22:21takriban 1451 KK

    huyo msichana ataletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo watu wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe. Amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kufanya ukahaba akiwa nyumbani kwa babaye. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

  13. Kumbukumbu 22:22takriban 1451 KK

    Ikiwa mwanaume atakutwa akizini na mke wa mtu mwingine, wote wawili, mwanaume na mwanamke aliyezini naye, lazima wauawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli.

  14. Kumbukumbu 22:23takriban 1451 KK

    Ikiwa mwanaume atakutana na bikira mjini ambaye ameposwa na mtu akazini naye,

  15. Kumbukumbu 22:24takriban 1451 KK

    utawachukua wote wawili kwenye lango la mji na kuwapiga kwa mawe mpaka wafe; yule msichana kwa kuwa alikuwa mjini na hakupiga kelele kuomba msaada, na yule mwanaume kwa sababu amemtenda jeuri mke wa mtu mwingine. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

  16. Kumbukumbu 22:25takriban 1451 KK

    Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa.

  17. Kumbukumbu 22:26takriban 1451 KK

    Usimtendee msichana yule jambo lolote; hajafanya dhambi inayostahili kifo. Shauri hili ni kama lile la yeyote ambaye anamshambulia na kumuua kwa makusudi jirani yake,

  18. Kumbukumbu 22:27takriban 1451 KK

    kwa maana mwanaume huyo alimkuta msichana huko mashambani, na ingawa msichana aliyeposwa alipiga kelele, hapakuwa na mtu wa kumwokoa.

  19. Kumbukumbu 22:28takriban 1451 KK

    Ikiwa itatokea mwanaume akutane na bikira ambaye hajaposwa na kumbaka nao wakakutwa,

  20. Kumbukumbu 22:29takriban 1451 KK

    mwanaume atamlipa baba wa msichana shekeli hamsini za fedha. Ni lazima amwoe huyo msichana, kwa maana amemfanyia jeuri. Kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

  21. Kumbukumbu 22:30takriban 1451 KK

    Mwanaume asimwoe mke wa baba yake; kamwe asidhalilishe kitanda cha baba yake.

  22. Kumbukumbu 23:1takriban 1451 KK

    Asiingie mtu yeyote aliyehasiwa kwa kupondwa makende au kwa kukatwa uume wake katika kusanyiko la Bwana.

  23. Kumbukumbu 23:2takriban 1451 KK

    Mtu yeyote ambaye amezaliwa kwenye ndoa isiyo halali au wazao wake wasiingie kwenye kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

  24. Kumbukumbu 23:3takriban 1451 KK

    Hapatakuwa na Mwamoni au Mmoabu au yeyote wa wazao wao atakayeruhusiwa kuingia katika kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

  25. Kumbukumbu 23:4takriban 1451 KK

    Kwa kuwa hawakuja kuwalaki wakiwa na mkate na maji mlipokuwa njiani mlipotoka Misri, tena walimwajiri Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyoko Aramu-Naharaimu ili kuwalaani ninyi.