Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kumbukumbu 23:5takriban 1451 KK

    Hata hivyo, Bwana Mungu wenu hakumsikiliza Balaamu bali aligeuza laana kuwa baraka kwenu kwa sababu Bwana Mungu wenu anawapenda.

  2. Kumbukumbu 23:6takriban 1451 KK

    Msitafute mapatano ya urafiki nao maisha yenu yote.

  3. Kumbukumbu 23:7takriban 1451 KK

    Usimchukie Mwedomu, kwa kuwa yeye ni ndugu yako. Usimchukie Mmisri, kwa sababu uliishi kama mgeni katika nchi yake.

  4. Kumbukumbu 23:8takriban 1451 KK

    Kizazi cha tatu cha watoto watakaozaliwa nao wanaweza kuingia katika kusanyiko la Bwana.

  5. Kumbukumbu 23:9takriban 1451 KK

    Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu chochote kisicho safi.

  6. Kumbukumbu 23:10takriban 1451 KK

    Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko.

  7. Kumbukumbu 23:11takriban 1451 KK

    Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini.

  8. Kumbukumbu 23:12takriban 1451 KK

    Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia.

  9. Kumbukumbu 23:13takriban 1451 KK

    Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho.

  10. Kumbukumbu 23:14takriban 1451 KK

    Kwa kuwa Bwana Mungu wenu hutembea katika kambi yenu ili kuwalinda na kuwaweka adui zenu mikononi mwenu. Kambi yenu ni lazima iwe takatifu, ili asione kitu chochote miongoni mwenu kilicho kichafu akageuka na kuwaacha.

  11. Kumbukumbu 23:15takriban 1451 KK

    Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake.

  12. Kumbukumbu 23:16takriban 1451 KK

    Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimwonee.

  13. Kumbukumbu 23:17takriban 1451 KK

    Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.

  14. Kumbukumbu 23:18takriban 1451 KK

    Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba ya Bwana Mungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababu Bwana Mungu wako anachukizwa na yote mawili.

  15. Kumbukumbu 23:19takriban 1451 KK

    Usimtoze ndugu yako riba, iwe ni fedha ama chakula ama kitu kingine chochote ambacho waweza kupata riba juu yake.

  16. Kumbukumbu 23:20takriban 1451 KK

    Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwamba Bwana Mungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki.

  17. Kumbukumbu 23:21takriban 1451 KK

    Ukiweka nadhiri kwa Bwana Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi.

  18. Kumbukumbu 23:22takriban 1451 KK

    Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia.

  19. Kumbukumbu 23:23takriban 1451 KK

    Chochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele za Bwana Mungu wako kwa kinywa chako mwenyewe.

  20. Kumbukumbu 23:24takriban 1451 KK

    Kama ukiingia katika shamba la mizabibu la jirani yako, unaweza kula zabibu kadiri utakavyo, lakini usiweke chochote kwenye kikapu chako.

  21. Kumbukumbu 23:25takriban 1451 KK

    Kama ukiingia katika shamba la nafaka la jirani yako, unaweza kukwanyua kwa mikono yako, lakini usikate kwa mundu nafaka iliyosimama.

  22. Kumbukumbu 24:1takriban 1451 KK

    Ikiwa mtu atamwoa mke na akamchukia kwa sababu ya kukosa adabu, naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake,

  23. Kumbukumbu 24:2takriban 1451 KK

    ikiwa baada ya kuondoka nyumbani kwake atakuwa mke wa mtu mwingine,

  24. Kumbukumbu 24:3takriban 1451 KK

    ikiwa mume wake wa pili atachukizwa naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake, au kama akifa,

  25. Kumbukumbu 24:4takriban 1451 KK

    basi yule mume wake wa kwanza, ambaye alimpa talaka, haruhusiwi kumwoa tena baada ya mwanamke huyo kuwa najisi. Hayo yatakuwa machukizo machoni pa Bwana. Usilete dhambi juu ya nchi ambayo Bwana Mungu wako anakupa kama urithi.