Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 13:56takriban 31 BK

    Nao dada zake wote, hawako hapa pamoja nasi? Mtu huyu amepata wapi basi mambo haya yote?”

  2. Mathayo 13:57takriban 31 BK

    Wakachukizwa naye. Lakini Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani kwake.”

  3. Mathayo 13:58takriban 31 BK

    Naye hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.

  4. Mathayo 14:1takriban 32 BK

    Wakati huo, Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za Yesu,

  5. Mathayo 14:2takriban 32 BK

    akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji; amefufuka kutoka kwa wafu! Hii ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

  6. Mathayo 14:3takriban 32 BK

    Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake,

  7. Mathayo 14:4takriban 32 BK

    kwa kuwa Yohana alikuwa amemwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.”

  8. Mathayo 14:5takriban 32 BK

    Herode alitaka sana kumuua Yohana, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii.

  9. Mathayo 14:6takriban 32 BK

    Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria, akamfurahisha sana Herode,

  10. Mathayo 14:7takriban 32 BK

    kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti chochote angeomba.

  11. Mathayo 14:8takriban 32 BK

    Huyo binti, akiwa amechochewa na mama yake, akasema, “Nipe kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.”

  12. Mathayo 14:9takriban 32 BK

    Mfalme akasikitika, lakini kwa sababu ya viapo alivyoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake.

  13. Mathayo 14:10takriban 32 BK

    Hivyo akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani.

  14. Mathayo 14:11takriban 32 BK

    Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.

  15. Mathayo 14:12takriban 32 BK

    Wanafunzi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wake kwenda kuuzika. Kisha wakaenda wakamwambia Yesu.

  16. Mathayo 14:13takriban 32 BK

    Yesu aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji.

  17. Mathayo 14:14takriban 32 BK

    Yesu alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.

  18. Mathayo 14:15takriban 32 BK

    Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”

  19. Mathayo 14:16takriban 32 BK

    Yesu akawaambia, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.”

  20. Mathayo 14:17takriban 32 BK

    Wakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”

  21. Mathayo 14:18takriban 32 BK

    Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.”

  22. Mathayo 14:19takriban 32 BK

    Yesu akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano.

  23. Mathayo 14:20takriban 32 BK

    Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili.

  24. Mathayo 14:21takriban 32 BK

    Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.

  25. Mathayo 14:22takriban 32 BK

    Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda ngʼambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano.