Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 13:31takriban 31 BK

    Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa Mbinguni ni kama punje ya haradali, ambayo mtu aliichukua, akaipanda shambani mwake.

  2. Mathayo 13:32takriban 31 BK

    Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hadi ndege wa angani wanakuja na kutengeneza viota katika matawi yake.”

  3. Mathayo 13:33takriban 31 BK

    Akawaambia mfano mwingine, “Ufalme wa Mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.”

  4. Mathayo 13:34takriban 31 BK

    Yesu alinena mambo haya yote kwa makutano kwa mifano. Wala hakuwaambia lolote pasipo mfano.

  5. Mathayo 13:35takriban 31 BK

    Hii ilikuwa ili kutimiza lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii aliposema: “Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano; nitahubiri mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.”

  6. Mathayo 13:36takriban 31 BK

    Kisha Yesu akaagana na makutano, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.”

  7. Mathayo 13:37takriban 31 BK

    Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.

  8. Mathayo 13:38takriban 31 BK

    Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa Ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu.

  9. Mathayo 13:39takriban 31 BK

    Yule adui aliyepanda magugu ni ibilisi. Mavuno ni mwisho wa dunia, nao wavunaji ni malaika.

  10. Mathayo 13:40takriban 31 BK

    “Kama vile magugu yangʼolewavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia.

  11. Mathayo 13:41takriban 31 BK

    Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote.

  12. Mathayo 13:42takriban 31 BK

    Nao watawatupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.

  13. Mathayo 13:43takriban 31 BK

    Ndipo wenye haki watangʼaa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio, na asikie.

  14. Mathayo 13:44takriban 31 BK

    “Ufalme wa Mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.”

  15. Mathayo 13:45takriban 31 BK

    “Tena, Ufalme wa Mbinguni unafanana na mfanyabiashara aliyekuwa akitafuta lulu safi.

  16. Mathayo 13:46takriban 31 BK

    Alipoipata lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza vyote alivyokuwa navyo akainunua.”

  17. Mathayo 13:47takriban 31 BK

    “Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama wavu wa kuvua samaki uliotupwa baharini ukavua samaki wa kila aina.

  18. Mathayo 13:48takriban 31 BK

    Ulipojaa, wavuvi wakavuta pwani, wakaketi na kukusanya samaki wazuri kuwaweka kwenye vyombo safi, lakini wale samaki wabaya wakawatupa.

  19. Mathayo 13:49takriban 31 BK

    Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki.

  20. Mathayo 13:50takriban 31 BK

    Nao watawatupa hao waovu katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.”

  21. Mathayo 13:51takriban 31 BK

    Yesu akauliza, “Je, mmeyaelewa haya yote?” Wakamjibu, “Ndiyo.”

  22. Mathayo 13:52takriban 31 BK

    Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa sheria aliyefundishwa elimu ya Ufalme wa Mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka ghala yake mali mpya na mali ya zamani.”

  23. Mathayo 13:53takriban 31 BK

    Yesu alipomaliza kutoa mifano hii, akaondoka.

  24. Mathayo 13:54takriban 31 BK

    Alipofika mji wa kwao, akawafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza?”

  25. Mathayo 13:55takriban 31 BK

    “Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si yeye aitwaye Maria, nao ndugu zake si Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda?