Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 14:23takriban 32 BK

    Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa huko peke yake.

  2. Mathayo 14:24takriban 32 BK

    Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.

  3. Mathayo 14:25takriban 32 BK

    Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji.

  4. Mathayo 14:26takriban 32 BK

    Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa.

  5. Mathayo 14:27takriban 32 BK

    Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.”

  6. Mathayo 14:28takriban 32 BK

    Petro akamjibu, “Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.”

  7. Mathayo 14:29takriban 32 BK

    Yesu akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu.

  8. Mathayo 14:30takriban 32 BK

    Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”

  9. Mathayo 14:31takriban 32 BK

    Mara Yesu akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?”

  10. Mathayo 14:32takriban 32 BK

    Nao walipoingia ndani ya mashua, upepo ukakoma.

  11. Mathayo 14:33takriban 32 BK

    Ndipo wote waliokuwa ndani ya ile mashua wakamwabudu Yesu, wakisema, “Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”

  12. Mathayo 14:34takriban 32 BK

    Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti.

  13. Mathayo 14:35takriban 32 BK

    Watu wa eneo lile walipomtambua Yesu, walipeleka habari sehemu zote za jirani. Watu wakamletea wagonjwa wao wote,

  14. Mathayo 14:36takriban 32 BK

    wakamsihi awaruhusu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake, nao wote waliomgusa, wakaponywa.

  15. Mathayo 15:1takriban 32 BK

    Ndipo baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamjia Yesu kutoka Yerusalemu na kumuuliza,

  16. Mathayo 15:2takriban 32 BK

    “Mbona wanafunzi wako wanakiuka mapokeo ya wazee? Kwa maana wao hawanawi mikono yao kabla ya kula!”

  17. Mathayo 15:3takriban 32 BK

    Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?

  18. Mathayo 15:4takriban 32 BK

    Kwa maana Mungu alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’

  19. Mathayo 15:5takriban 32 BK

    Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,’

  20. Mathayo 15:6takriban 32 BK

    basi hana tena sababu ya kumheshimu baba yake nacho. Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu.

  21. Mathayo 15:7takriban 32 BK

    Ninyi wanafiki! Isaya alikuwa sawa alipotabiri juu yenu kwamba:

  22. Mathayo 15:8takriban 32 BK

    “ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.

  23. Mathayo 15:9takriban 32 BK

    Huniabudu bure; nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’ ”

  24. Mathayo 15:10takriban 32 BK

    Yesu akaita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni na mwelewe:

  25. Mathayo 15:11takriban 32 BK

    kinachomfanya mtu kuwa najisi mbele za Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.”