Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yohana 7:42takriban 33 BK

    Je, Maandiko hayasemi kwamba Kristo atakuja kutoka jamaa ya Daudi na kutoka Bethlehemu, mji alioishi Daudi?”

  2. Yohana 7:43takriban 33 BK

    Kwa hiyo watu wakagawanyika kwa ajili ya Yesu.

  3. Yohana 7:44takriban 33 BK

    Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa.

  4. Yohana 7:45takriban 33 BK

    Hatimaye wale walinzi wa Hekalu wakarudi kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo waliokuwa wamewatuma ili kumkamata Yesu, wakaulizwa, “Mbona hamkumkamata?”

  5. Yohana 7:46takriban 33 BK

    Wale walinzi wakajibu, “Kamwe hajanena mtu yeyote kama yeye anenavyo.”

  6. Yohana 7:47takriban 33 BK

    Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika?

  7. Yohana 7:48takriban 33 BK

    Je, kuna kiongozi yeyote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini?

  8. Yohana 7:49takriban 33 BK

    Lakini huu umati wa watu wasiojua Sheria ya Mose, wamelaaniwa.”

  9. Yohana 7:50takriban 33 BK

    Ndipo Nikodemo, yule aliyekuwa amemwendea Yesu siku moja usiku, ambaye alikuwa mmoja wao akauliza,

  10. Yohana 7:51takriban 33 BK

    “Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?”

  11. Yohana 7:52takriban 33 BK

    Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza nawe utaona kwamba hakuna nabii atokae Galilaya!” [

  12. Yohana 7:53takriban 33 BK

    Kisha wakaondoka, kila mtu akarudi nyumbani kwake.

  13. Yohana 8:1takriban 33 BK

    Lakini Yesu akaenda katika Mlima wa Mizeituni.

  14. Yohana 8:2takriban 33 BK

    Alfajiri na mapema Yesu akaja tena Hekaluni, watu wote wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha.

  15. Yohana 8:3takriban 33 BK

    Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote.

  16. Yohana 8:4takriban 33 BK

    Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini.

  17. Yohana 8:5takriban 33 BK

    Katika sheria, Mose alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?”

  18. Yohana 8:6takriban 33 BK

    Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake.

  19. Yohana 8:7takriban 33 BK

    Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

  20. Yohana 8:8takriban 33 BK

    Akainama tena na kuandika ardhini.

  21. Yohana 8:9takriban 33 BK

    Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake.

  22. Yohana 8:10takriban 33 BK

    Yesu akainuka na kumwambia, “Wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?”

  23. Yohana 8:11takriban 33 BK

    Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja Bwana.” Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako, kuanzia sasa usitende dhambi tena.”]

  24. Yohana 8:12takriban 33 BK

    Kisha Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”

  25. Yohana 8:13takriban 33 BK

    Mafarisayo wakamwambia, “Ushuhuda wako haukubaliki kwa kuwa unajishuhudia mwenyewe.”