Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yohana 8:14takriban 33 BK

    Yesu akawajibu, “Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli kwa sababu najua nilikotoka na ninakokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakokwenda.

  2. Yohana 8:15takriban 33 BK

    Ninyi mnahukumu kwa kufuata vipimo vya kibinadamu, mimi simhukumu mtu yeyote.

  3. Yohana 8:16takriban 33 BK

    Lakini hata kama nikihukumu, uamuzi wangu ni sahihi kwa sababu sitoi hukumu yangu peke yangu, bali niko pamoja na Baba, aliyenituma.

  4. Yohana 8:17takriban 33 BK

    Imeandikwa katika Sheria yenu kwamba, ushahidi wa watu wawili ni thabiti.

  5. Yohana 8:18takriban 33 BK

    Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma hunishuhudia.”

  6. Yohana 8:19takriban 33 BK

    Ndipo wakamuuliza, “Huyo Baba yako yuko wapi?” Yesu akawajibu, “Ninyi hamnifahamu mimi ni nani, wala hammfahamu Baba yangu. Kama mngenifahamu mimi, mngemfahamu na Baba yangu.”

  7. Yohana 8:20takriban 33 BK

    Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika chumba cha hazina Hekaluni. Lakini hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa saa yake ilikuwa haijawadia.

  8. Yohana 8:21takriban 33 BK

    Yesu akawaambia tena, “Ninaenda zangu, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi ninyi hamwezi kuja.”

  9. Yohana 8:22takriban 33 BK

    Ndipo wale Wayahudi wakasema, “Je, atajiua? Je, hii ndiyo sababu amesema, ‘Niendako mimi ninyi hamwezi kuja’?”

  10. Yohana 8:23takriban 33 BK

    Akawaambia, “Ninyi mmetoka chini, mimi nimetoka juu. Ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.

  11. Yohana 8:24takriban 33 BK

    Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu, kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.”

  12. Yohana 8:25takriban 33 BK

    Wakamuuliza, “Wewe ni nani?” Naye Yesu akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nimekuwa nikiwaambia tangu mwanzo.

  13. Yohana 8:26takriban 33 BK

    Nina mambo mengi ya kusema juu yenu na mengi ya kuwahukumu. Lakini yeye aliyenituma ni wa kweli, nami nanena na ulimwengu niliyoyasikia kutoka kwake.”

  14. Yohana 8:27takriban 33 BK

    Hawakuelewa kuwa alikuwa akiwaambia juu ya Baba yake wa Mbinguni.

  15. Yohana 8:28takriban 33 BK

    Kisha Yesu akawaambia, “Mtakapokwisha kumwinua juu Mwana wa Adamu, ndipo mtakapojua kuwa, ‘Mimi ndiye yule niliyesema na kwamba mimi sitendi jambo lolote peke yangu bali ninasema yale tu ambayo Baba yangu amenifundisha.

  16. Yohana 8:29takriban 33 BK

    Yeye aliyenituma yu pamoja nami, hajaniacha, kwa kuwa siku zote nafanya mapenzi yake.’ ”

  17. Yohana 8:30takriban 33 BK

    Wengi waliomsikia Yesu akisema maneno haya wakamwamini.

  18. Yohana 8:31takriban 33 BK

    Kisha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli.

  19. Yohana 8:32takriban 33 BK

    Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”

  20. Yohana 8:33takriban 33 BK

    Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Abrahamu, nasi hatujawa watumwa wa mtu yeyote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?”

  21. Yohana 8:34takriban 33 BK

    Yesu akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.

  22. Yohana 8:35takriban 33 BK

    Mtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima.

  23. Yohana 8:36takriban 33 BK

    Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.

  24. Yohana 8:37takriban 33 BK

    Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Abrahamu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu.

  25. Yohana 8:38takriban 33 BK

    Ninasema yale niliyoyaona mbele za Baba yangu, nanyi inawapa kufanya yale mliyosikia kutoka kwa baba yenu.”