Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yohana 9:5takriban 33 BK

    Wakati niko ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.”

  2. Yohana 9:6takriban 33 BK

    Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule mtu kipofu machoni.

  3. Yohana 9:7takriban 33 BK

    Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.

  4. Yohana 9:8takriban 33 BK

    Majirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona hapo awali akiombaomba wakaanza kuuliza, “Je, huyu si yule aliyekuwa akiketi akiombaomba?”

  5. Yohana 9:9takriban 33 BK

    Wengine wakasema, “Ndiye.” Wengine wakasema, “Siye, bali wamefanana.” Lakini yeye akawaambia, “Mimi ndiye.”

  6. Yohana 9:10takriban 33 BK

    Wakamuuliza, “Basi macho yako yalifumbuliwaje?”

  7. Yohana 9:11takriban 33 BK

    Yeye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alitengeneza tope, akanipaka machoni mwangu, naye akaniambia nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu, ndipo nikanawa nami nikapata kuona!”

  8. Yohana 9:12takriban 33 BK

    Wale wakamuuliza, “Yeye huyo mtu yuko wapi?” Akawajibu, “Sijui.”

  9. Yohana 9:13takriban 33 BK

    Wakamleta kwa Mafarisayo yule mtu aliyekuwa kipofu hapo awali.

  10. Yohana 9:14takriban 33 BK

    Basi siku hiyo Yesu alipotengeneza tope na kuyafungua macho ya huyo mtu ilikuwa Sabato.

  11. Yohana 9:15takriban 33 BK

    Mafarisayo nao wakaanza kumuuliza alivyopata kuponywa. Naye akawaambia, “Alinipaka tope kwenye macho yangu, nikanawa na sasa ninaona.”

  12. Yohana 9:16takriban 33 BK

    Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Huyu mtu hatoki kwa Mungu, kwa sababu hashiki Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya miujiza kama hii?” Wakagawanyika.

  13. Yohana 9:17takriban 33 BK

    Hivyo wakamwambia tena yule mtu aliyekuwa kipofu, “Wewe ndiwe uliyefumbuliwa macho, wasemaje kuhusu mtu huyo?” Maana macho yako ndiyo yaliyofumbuliwa. Yeye akawajibu, “Yeye ni nabii.”

  14. Yohana 9:18takriban 33 BK

    Wale Wayahudi hawakuamini ya kuwa mtu huyo alikuwa kipofu, akapata kuona, mpaka walipowaita wazazi wake.

  15. Yohana 9:19takriban 33 BK

    Wakawauliza, “Je, huyu ni mtoto wenu, ambaye mnasema alizaliwa kipofu? Imekuwaje basi sasa anaona?”

  16. Yohana 9:20takriban 33 BK

    Wazazi wake wakajibu, “Tunajua ya kuwa huyu ni mtoto wetu na ya kuwa alizaliwa kipofu.

  17. Yohana 9:21takriban 33 BK

    Lakini sisi hatujui ni kwa jinsi gani kwamba sasa anaona, wala hatujui ni nani aliyemfungua macho yake. Muulizeni, yeye ni mtu mzima na anaweza kujieleza mwenyewe.”

  18. Yohana 9:22takriban 33 BK

    Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa Wayahudi kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakayemkiri Yesu kuwa ndiye Kristo atafukuzwa kutoka sinagogi.

  19. Yohana 9:23takriban 33 BK

    Kwa hiyo wazazi wake wakasema, “Yeye ni mtu mzima. Muulizeni.”

  20. Yohana 9:24takriban 33 BK

    Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.”

  21. Yohana 9:25takriban 33 BK

    Akawajibu, “Mimi sijui kama yeye ni mwenye dhambi. Lakini jambo moja ninalojua, nilikuwa kipofu na sasa ninaona.”

  22. Yohana 9:26takriban 33 BK

    Wakamuuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?”

  23. Yohana 9:27takriban 33 BK

    Akawajibu, “Tayari nimekwisha kuwaambia, nanyi hamtaki kunisikiliza. Mbona mnataka kusikia tena? Je, ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?”

  24. Yohana 9:28takriban 33 BK

    Ndipo wakamtukana na kusema, “Wewe ndiwe mwanafunzi wake, Sisi ni wanafunzi wa Mose.

  25. Yohana 9:29takriban 33 BK

    Tunajua kwamba Mungu alisema na Mose, lakini kwa habari ya mtu huyu hatujui atokako.”