Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yohana 10:14takriban 33 BK

    “Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua.

  2. Yohana 10:15takriban 33 BK

    Kama vile Baba anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.

  3. Yohana 10:16takriban 33 BK

    Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja.

  4. Yohana 10:17takriban 33 BK

    Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena.

  5. Yohana 10:18takriban 33 BK

    Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”

  6. Yohana 10:19takriban 33 BK

    Kwa maneno haya Wayahudi waligawanyika.

  7. Yohana 10:20takriban 33 BK

    Wengi wao wakasema, “Huyu amepagawa na pepo mchafu, naye amechanganyikiwa.”

  8. Yohana 10:21takriban 33 BK

    Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na pepo mchafu. Je, pepo mchafu aweza kufungua macho ya kipofu?”

  9. Yohana 10:22takriban 33 BK

    Wakati huo ilikuwa Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu huko Yerusalemu, nao ulikuwa wakati wa majira ya baridi.

  10. Yohana 10:23takriban 33 BK

    Naye Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Solomoni.

  11. Yohana 10:24takriban 33 BK

    Wayahudi wakamkusanyikia wakamuuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo tuambie waziwazi.”

  12. Yohana 10:25takriban 33 BK

    Yesu akawajibu, “Nimewaambia, lakini hamwamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yananishuhudia.

  13. Yohana 10:26takriban 33 BK

    Lakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu.

  14. Yohana 10:27takriban 33 BK

    Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata,

  15. Yohana 10:28takriban 33 BK

    nami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu.

  16. Yohana 10:29takriban 33 BK

    Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake.

  17. Yohana 10:30takriban 33 BK

    Mimi na Baba yangu tu umoja.”

  18. Yohana 10:31takriban 33 BK

    Kwa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo,

  19. Yohana 10:32takriban 33 BK

    lakini Yesu akawaambia, “Nimewaonyesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni ipi katika hiyo mnataka kunipiga mawe?”

  20. Yohana 10:33takriban 33 BK

    Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ingawa ni mwanadamu unajifanya kuwa Mungu.”

  21. Yohana 10:34takriban 33 BK

    Yesu akawajibu, “Je, haikuandikwa katika Sheria ya kwamba, ‘Nimesema kuwa, ninyi ni miungu?’

  22. Yohana 10:35takriban 33 BK

    Kama aliwaita ‘miungu,’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka,

  23. Yohana 10:36takriban 33 BK

    je, mwawezaje kusema kwamba yule ambaye Baba amemweka wakfu na kumtuma ulimwenguni anakufuru, kwa sababu nilisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu?’

  24. Yohana 10:37takriban 33 BK

    Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msiniamini,

  25. Yohana 10:38takriban 33 BK

    lakini ikiwa nazifanya kazi za Mungu, hata kama hamniamini mimi ziaminini hizo kazi, ili mpate kujua na kuelewa kwamba Baba yu ndani yangu, nami ndani yake.”