Rukia maudhui

circa 605–538 BC

The Babylonian Exile

Jerusalem falls and the temple burns; Ezekiel and Daniel minister among the exiles as Lamentations mourns the city's ruin.

1,784 mistari · 3 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Ezekieli 24:5takriban 590 KK

    chagua yule aliye bora wa kundi la kondoo. Panga kuni chini ya sufuria kwa ajili ya mifupa; chochea mpaka ichemke na uitokose hiyo mifupa ndani yake.

  2. Ezekieli 24:6takriban 590 KK

    “ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ole wa mji umwagao damu, ole wa sufuria ambayo sasa ina ukoko ndani yake, ambayo ukoko wake hautoki. Kipakue kipande baada ya kipande, bila kuvipigia kura.

  3. Ezekieli 24:7takriban 590 KK

    “ ‘Kwa kuwa damu aliyoimwaga ipo katikati yake: huyo mwanamke aliimwaga juu ya mwamba ulio wazi; hakuimwaga kwenye ardhi, ambako vumbi lingeifunika.

  4. Ezekieli 24:8takriban 590 KK

    Kuchochea ghadhabu na kulipiza kisasi, nimemwaga damu yake juu ya mwamba ulio wazi, ili isifunikwe.

  5. Ezekieli 24:9takriban 590 KK

    “ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ole wa mji umwagao damu! Mimi nami nitalundikia kuni nyingi.

  6. Ezekieli 24:10takriban 590 KK

    Kwa hiyo lundika kuni na uwashe moto. Pika hiyo nyama vizuri, changanya viungo ndani yake, na uiache mifupa iungue kwenye moto.

  7. Ezekieli 24:11takriban 590 KK

    Kisha teleka sufuria tupu kwenye makaa mpaka iwe na moto sana na shaba yake ingʼae, ili uchafu wake upate kuyeyuka na ukoko wake upate kuungua na kuondoka.

  8. Ezekieli 24:12takriban 590 KK

    Imezuia juhudi zote, ukoko wake mwingi haujaondoka, hata ikiwa ni kwa moto.

  9. Ezekieli 24:13takriban 590 KK

    “ ‘Sasa uchafu wako ni uasherati wako. Kwa sababu nilijaribu kukutakasa lakini haikuwezekana kutakaswa kutoka kwenye huo uchafu wako, hutatakasika tena mpaka ghadhabu yangu dhidi yako iwe imepungua.

  10. Ezekieli 24:14takriban 590 KK

    “ ‘Mimi Bwana nimesema, wakati umewadia wa mimi kutenda. Mimi sitazuia, mimi sitaona huruma wala sitapunguza hasira yangu, Utahukumiwa sawasawa na mwenendo na matendo yako, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

  11. Ezekieli 24:15takriban 590 KK

    Neno la Bwana likanijia kusema:

  12. Ezekieli 24:16takriban 590 KK

    “Mwanadamu, kwa pigo moja nakaribia kukuondolea kile kilicho furaha ya macho yako. Lakini usiomboleze au kulia wala kudondosha machozi yoyote.

  13. Ezekieli 24:17takriban 590 KK

    Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya kawaida vya wakati wa matanga.”

  14. Ezekieli 24:18takriban 590 KK

    Hivyo nikanena na watu asubuhi na jioni mke wangu akafa. Asubuhi yake nilifanya kama nilivyoamriwa.

  15. Ezekieli 24:19takriban 590 KK

    Ndipo watu wakaniuliza, “Je, jambo hili unalofanya linamaanisha nini kwetu?”

  16. Ezekieli 24:20takriban 590 KK

    Kwa hiyo nikawaambia, “Neno la Bwana lilinijia kusema:

  17. Ezekieli 24:21takriban 590 KK

    ‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu na binti zenu mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga.

  18. Ezekieli 24:22takriban 590 KK

    Nanyi mtafanya kama nilivyofanya. Hamtafunika sehemu ya chini ya nyuso zenu wala hamtakula vyakula vya kawaida vya waombolezaji.

  19. Ezekieli 24:23takriban 590 KK

    Mtajifunga vilemba vichwani mwenu na kuvaa viatu vyenu miguuni mwenu. Hamtaomboleza au kulia, lakini mtadhoofika kwa sababu ya dhambi zenu na kulia kwa uchungu kila mtu na mwenzake.

  20. Ezekieli 24:24takriban 590 KK

    Ezekieli atakuwa ishara kwenu, mtafanya kama yeye alivyofanya. Wakati jambo hili litakapotokea, mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.’

  21. Ezekieli 24:25takriban 590 KK

    “Nawe, mwanadamu, siku ile nitakapoondoa ngome yao iliyo furaha yao na utukufu wao, kitu cha kupendeza macho yao, kile kilicho shauku ya mioyo yao, wana wao na binti zao vilevile,

  22. Ezekieli 24:26takriban 590 KK

    siku hiyo atakayetoroka atakuja kuwapasha habari.

  23. Ezekieli 24:27takriban 590 KK

    Katika siku ile kinywa chako kitamfumbukia yeye aliyenusurika, nawe utaongea wala hutanyamaza tena. Hivyo wewe utakuwa ishara kwao, nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.”

  24. Ezekieli 25:1takriban 590 KK

    Neno la Bwana likanijia kusema:

  25. Ezekieli 25:2takriban 590 KK

    “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Waamoni utabiri dhidi yao.