Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Waefeso 4:9takriban 64 BK

    (Asemapo “alipaa juu,” maana yake nini isipokuwa ni kusema pia kwamba Kristo alishuka pande za chini sana za dunia?

  2. Waefeso 4:10takriban 64 BK

    Yeye aliyeshuka ndiye alipaa juu zaidi kupita mbingu zote, ili apate kuujaza ulimwengu wote.)

  3. Waefeso 4:11takriban 64 BK

    Ndiye aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu,

  4. Waefeso 4:12takriban 64 BK

    kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate kujengwa

  5. Waefeso 4:13takriban 64 BK

    mpaka sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua sana Mwana wa Mungu na kuwa watu wazima kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Kristo.

  6. Waefeso 4:14takriban 64 BK

    Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu.

  7. Waefeso 4:15takriban 64 BK

    Badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo, katika mambo yote tukue, hata tumfikie yeye aliye kichwa, yaani, Kristo.

  8. Waefeso 4:16takriban 64 BK

    Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeungamanishwa na kushikamanishwa pamoja kwa msaada wa kila kiungo, hukua na kujijenga wenyewe katika upendo, wakati kila kiungo kinafanya kazi yake.

  9. Waefeso 4:17takriban 64 BK

    Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao.

  10. Waefeso 4:18takriban 64 BK

    Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao.

  11. Waefeso 4:19takriban 64 BK

    Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.

  12. Waefeso 4:20takriban 64 BK

    Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Kristo.

  13. Waefeso 4:21takriban 64 BK

    Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu.

  14. Waefeso 4:22takriban 64 BK

    Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu,

  15. Waefeso 4:23takriban 64 BK

    ili mfanywe upya roho na nia zenu,

  16. Waefeso 4:24takriban 64 BK

    mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.

  17. Waefeso 4:25takriban 64 BK

    Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja.

  18. Waefeso 4:26takriban 64 BK

    Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika,

  19. Waefeso 4:27takriban 64 BK

    wala msimpe ibilisi nafasi.

  20. Waefeso 4:28takriban 64 BK

    Yeye ambaye amekuwa akiiba, asiibe tena, lakini lazima ajishughulishe, afanye kitu kifaacho kwa mikono yake mwenyewe, ili awe na kitu cha kuwagawia wahitaji.

  21. Waefeso 4:29takriban 64 BK

    Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao.

  22. Waefeso 4:30takriban 64 BK

    Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.

  23. Waefeso 4:31takriban 64 BK

    Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu.

  24. Waefeso 4:32takriban 64 BK

    Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

  25. Waefeso 5:1takriban 64 BK

    Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto wapendwao,