Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Waefeso 3:5takriban 64 BK

    Siri hii haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu.

  2. Waefeso 3:6takriban 64 BK

    Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu wa Mataifa ni warithi pamoja na Israeli, viungo vya mwili mmoja na washiriki pamoja wa ahadi katika Kristo Yesu.

  3. Waefeso 3:7takriban 64 BK

    Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi.

  4. Waefeso 3:8takriban 64 BK

    Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii: ili niwahubirie watu wa Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo,

  5. Waefeso 3:9takriban 64 BK

    na kuweka wazi kwa kila mtu siri hii iliyokuwa imefichwa tangu zamani katika Mungu, aliyeumba vitu vyote.

  6. Waefeso 3:10takriban 64 BK

    Ili sasa kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na wenye mamlaka katika ulimwengu wa roho,

  7. Waefeso 3:11takriban 64 BK

    sawasawa na kusudi lake la milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

  8. Waefeso 3:12takriban 64 BK

    Ndani yake na kwa njia ya imani katika yeye twaweza kumkaribia Mungu kwa uhuru na kwa ujasiri.

  9. Waefeso 3:13takriban 64 BK

    Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni utukufu wenu.

  10. Waefeso 3:14takriban 64 BK

    Kwa sababu hii nampigia Baba magoti,

  11. Waefeso 3:15takriban 64 BK

    ambaye ubaba wote wa kila jamaa za mbinguni na za duniani unatokana naye.

  12. Waefeso 3:16takriban 64 BK

    Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake,

  13. Waefeso 3:17takriban 64 BK

    ili kwamba, Kristo apate kukaa mioyoni mwenu kwa njia ya imani. Nami ninaomba kwamba ninyi mkiwa wenye mizizi tena imara katika msingi wa upendo,

  14. Waefeso 3:18takriban 64 BK

    mwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, urefu, kimo na kina upendo wa Kristo,

  15. Waefeso 3:19takriban 64 BK

    na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu.

  16. Waefeso 3:20takriban 64 BK

    Basi kwa yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza wake ule utendao kazi ndani yetu,

  17. Waefeso 3:21takriban 64 BK

    yeye atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen.

  18. Waefeso 4:1takriban 64 BK

    Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa.

  19. Waefeso 4:2takriban 64 BK

    Kwa unyenyekevu wote na upole, mkiwa wavumilivu, mkichukuliana kwa upendo.

  20. Waefeso 4:3takriban 64 BK

    Jitahidini kudumisha umoja wa Roho katika kifungo cha amani.

  21. Waefeso 4:4takriban 64 BK

    Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja.

  22. Waefeso 4:5takriban 64 BK

    Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,

  23. Waefeso 4:6takriban 64 BK

    Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote.

  24. Waefeso 4:7takriban 64 BK

    Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo.

  25. Waefeso 4:8takriban 64 BK

    Kwa hiyo husema: “Alipopaa juu zaidi, aliteka mateka, akawapa wanadamu vipawa.”