Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Trust

109 mistari · 66 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Uyalinde maisha yangu na uniokoe, usiniache niaibike, kwa maana nimekukimbilia wewe.

  2. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, nithibitishe katika haki, maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; nimemtumainia Bwana bila kusitasita.

  3. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe, kwa haki yako uniokoe.

  4. Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana; nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.”

  5. Mtu mwovu ana taabu nyingi, bali upendo usio na kikomo wa Bwana unamzunguka mtu anayemtumaini.

  6. Mioyo yetu humshangilia, kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.

  7. Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia.

  8. Bwana huwakomboa watumishi wake, yeyote anayemkimbilia yeye hatahukumiwa kamwe.

  9. Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako.

  10. Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema; Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

  11. Mkabidhi Bwana njia yako, mtumaini yeye, naye atatenda hili:

  12. Bwana huwasaidia na kuwaokoa, huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi, kwa maana wanamkimbilia.

  13. Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo.

  14. Siutumaini upinde wangu, upanga wangu hauniletei ushindi;

  15. wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi?

  16. “Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake, na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”

  17. Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni unaostawi katika nyumba ya Mungu, nautegemea upendo wa Mungu usiokoma milele na milele.

  18. katika Mungu ninatumaini, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

  19. Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote, miminieni mioyo yenu kwake, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.

  20. Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki, Ee Mungu Mwokozi wetu, tumaini la miisho yote ya duniani na la bahari zilizo mbali sana,

  21. Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu.

  22. kwa kuwa hawakumwamini Mungu, wala kuutumainia ukombozi wake.

  23. Mikononi mwao watakuinua, ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.

  24. Hataogopa habari mbaya, moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.

  25. Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.