Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Seekers

165 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Maskini wataona na kufurahi: ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!

  2. Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu na atukuzwe!”

  3. Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Ee Mungu, unijie haraka. Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Ee Bwana, usikawie.

  4. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu. Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie.

  5. Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijika.

  6. Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni; nikatafakari, roho yangu ikadhoofika.

  7. Ulizuia macho yangu kufumba; nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema.

  8. Nilitafakari juu ya siku zilizopita, miaka mingi iliyopita,

  9. nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku. Moyo wangu ulitafakari na roho yangu ikauliza:

  10. “Je, Bwana atakataa milele? Je, hatatenda mema tena?

  11. Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? Je, ahadi yake imekoma nyakati zote?

  12. Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?”

  13. Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku.

  14. Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza.

  15. Funika nyuso zao kwa aibu ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana.

  16. Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za Bwana; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai.

  17. Mtafuteni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.

  18. Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote.

  19. Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.

  20. Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.

  21. Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.

  22. Nanyoosha mikono yangu kwako, nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame.

  23. Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.

  24. Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.

  25. na kama ukiita busara na kuita kwa sauti ufahamu,