Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Seekers

165 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Hiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao, wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

  2. niongoze katika kweli yako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.

  3. Macho yangu humwelekea Bwana daima, kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa miguu yangu kutoka mtego.

  4. Jambo moja ninamwomba Bwana, hili ndilo ninalolitafuta: niweze kukaa nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana na kumtafuta hekaluni mwake.

  5. Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, Bwana “Nitautafuta.”

  6. Mngojee Bwana, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee Bwana.

  7. Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu.

  8. Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.

  9. Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu chochote kilicho chema.

  10. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Nilimngoja Bwana kwa saburi, naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

  11. Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, kutoka matope na utelezi; akaiweka miguu yangu juu ya mwamba na kunipa mahali imara pa kusimama.

  12. Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa na kuweka tumaini lao kwa Bwana.

  13. Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo.

  14. Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora. Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu.

  15. Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?

  16. Machozi yangu yamekuwa chakula changu usiku na mchana, huku watu wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?”

  17. Mambo haya nayakumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, kwa kelele za shangwe na za shukrani katikati ya umati uliosherehekea.

  18. Zaburi ya Daudi. Wakati alipokuwa katika Jangwa la Yuda. Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka mahali ambapo hapana maji.

  19. Nimekuona katika mahali patakatifu na kuuona uwezo wako na utukufu wako.

  20. Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakuadhimisha.

  21. Nitakusifu siku zote za maisha yangu, na kwa jina lako nitainua mikono yangu.

  22. Nafsi yangu itatoshelezwa kama kwa wingi wa vyakula; kwa midomo iimbayo kinywa changu kitakusifu wewe.

  23. Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.

  24. Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.

  25. Nafsi yangu inaambatana nawe, mkono wako wa kuume hunishika.