Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Priests: Divided by David into twenty-four courses

22 mistari · 86 vipengele

Mistari kuhusu Divided by David into twenty-four courses

  1. Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni: Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

  2. Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani.

  3. Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao.

  4. Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari.

  5. Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

  6. Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.

  7. Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu, ya pili Yedaya,

  8. ya tatu Harimu, ya nne Seorimu,

  9. ya tano Malkiya, ya sita Miyamini,

  10. ya saba Hakosi, ya nane Abiya,

  11. ya tisa Yeshua, ya kumi Shekania,

  12. ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu,

  13. ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu,

  14. ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri,

  15. ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi,

  16. ya kumi na tisa Pethahia, ya ishirini Yehezkeli,

  17. ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli,

  18. ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia.

  19. Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

  20. Kwa kushika maagizo ya Daudi baba yake, aliweka migawanyo ya makuhani kwa ajili ya kazi zao, nao Walawi kuongoza kusifu na kusaidia makuhani kufuatana na mahitaji ya kila siku. Pia akaweka mabawabu katika migawanyo kwa ajili ya malango mbalimbali, kwa sababu hili ndilo Daudi mtu wa Mungu alilokuwa ameagiza.

  21. Jiandaeni kwa kufuata jamaa zenu katika migawanyo yenu, kufuatana na maelezo yaliyoandikwa na Daudi mfalme wa Israeli na mwanawe Solomoni.

  22. “Simameni mahali patakatifu kwa kufuata migawanyo ya jamaa za baba zenu kulingana na koo zenu na pawepo Walawi kwa ajili ya kila mgawanyo wa nyumba ya baba zenu.