Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Peter: His perfidy foretold by Jesus, and his profession of fidelity

13 mistari · 35 vipengele

Mistari kuhusu His perfidy foretold by Jesus, and his profession of fidelity

  1. Petro akajibu, “Hata kama wote watakuacha, kamwe mimi sitakuacha.”

  2. Yesu akamjibu, “Amin, nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”

  3. Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wanafunzi wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.

  4. Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.”

  5. Yesu akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.”

  6. Lakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.

  7. Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano.

  8. Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.”

  9. Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani na hata kifoni.”

  10. Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika usiku wa leo, utakana mara tatu kwamba hunijui mimi.”

  11. Simoni Petro akamuuliza, “Bwana, unakwenda wapi?” Yesu akamjibu, “Ninakokwenda huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.”

  12. Petro akamuuliza tena, “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Mimi niko tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako.”

  13. Yesu akamjibu, “Je, ni kweli uko tayari kuutoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin nakuambia, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”