Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Peter: Called Simon Bar-Jona and Cephas

6 mistari · 35 vipengele

Mistari kuhusu Called Simon Bar-Jona and Cephas

  1. Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”

  2. Naye Yesu akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona,kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni.

  3. Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda.

  4. Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”

  5. Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro);

  6. Naye akamleta kwa Yesu. Yesu akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa” (ambalo limetafsiriwa Petro).