Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Nation

183 mistari · 11 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki.

  2. Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.

  3. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.

  4. Ulisamehe uovu wa watu wako, na kufunika dhambi zao zote.

  5. Uliweka kando ghadhabu yako yote na umegeuka na kuiacha hasira yako kali.

  6. Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, nawe uiondoe chuki yako juu yetu.

  7. Je, utatukasirikia milele? Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote?

  8. Je, hutatuhuisha tena, ili watu wako wakufurahie?

  9. Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana, utupe wokovu wako.

  10. Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, wanaotembea katika mwanga wa uwepo wako, Ee Bwana.

  11. Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, wanafurahi katika haki yako.

  12. Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, kwa wema wako unatukuza pembe yetu.

  13. Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana, na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.

  14. nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

  15. kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako na huwabariki watu wako walio ndani yako.

  16. Huwapa amani mipakani mwenu na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.

  17. Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu kwa watu wote.

  18. wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia, wakati wa vita na wakati wa amani.

  19. Atahukumu kati ya mataifa na ataamua migogoro ya mataifa mengi. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena.

  20. utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli: Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho! Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma!

  21. Bwana amevunja fimbo ya mwovu, fimbo ya utawala ya watawala,

  22. ambayo kwa hasira waliyapiga mataifa kwa mapigo yasiyo na kikomo, nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifa kwa jeuri pasipo huruma.

  23. Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani, wanabubujika kwa kuimba.

  24. Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote, huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote.

  25. Kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amekusudia, ni nani awezaye kumzuia? Mkono wake umenyooshwa, ni nani awezaye kuurudisha?