Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kumbukumbu 5:27takriban 1451 KK

    Sogea karibu usikie yale yote asemayo Bwana Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho Bwana Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”

  2. Kumbukumbu 5:28takriban 1451 KK

    Bwana aliwasikia wakati mlipozungumza nami, na Bwana akaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri.

  3. Kumbukumbu 5:29takriban 1451 KK

    Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele!

  4. Kumbukumbu 5:30takriban 1451 KK

    “Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao.

  5. Kumbukumbu 5:31takriban 1451 KK

    Lakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.”

  6. Kumbukumbu 5:32takriban 1451 KK

    Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yale Bwana Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto.

  7. Kumbukumbu 5:33takriban 1451 KK

    Fuateni yale yote ambayo Bwana Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.

  8. Kumbukumbu 6:1takriban 1451 KK

    Haya ndiyo maagizo, amri na sheria ambazo Bwana Mungu wenu aliniagiza niwafundishe ninyi ili mpate kuyashika katika nchi ambayo ninyi mnavuka Yordani kuimiliki,

  9. Kumbukumbu 6:2takriban 1451 KK

    ili kwamba ninyi, watoto wenu na watoto wao baada yao wamche Bwana Mungu wenu siku zote kwa kushika amri na maagizo yake yote ninayowapa, ili mweze kuyafurahia maisha marefu.

  10. Kumbukumbu 6:3takriban 1451 KK

    Sikia, ee Israeli, nawe uwe mwangalifu kutii ili upate kufanikiwa na kuongezeka sana katika nchi itiririkayo maziwa na asali, kama Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi ninyi.

  11. Kumbukumbu 6:4takriban 1451 KK

    Sikia, ee Israeli: Bwana Mungu wako, Bwana ni mmoja.

  12. Kumbukumbu 6:5takriban 1451 KK

    Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

  13. Kumbukumbu 6:6takriban 1451 KK

    Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako.

  14. Kumbukumbu 6:7takriban 1451 KK

    Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

  15. Kumbukumbu 6:8takriban 1451 KK

    Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako.

  16. Kumbukumbu 6:9takriban 1451 KK

    Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.

  17. Kumbukumbu 6:10takriban 1451 KK

    Wakati Bwana Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia baba zako, Abrahamu, Isaki na Yakobo, kukupa wewe, nchi kubwa, ina miji inayopendeza ambayo hukuijenga,

  18. Kumbukumbu 6:11takriban 1451 KK

    nyumba zilizojaa vitu vizuri vya aina nyingi ambavyo hukuvijaza, visima ambavyo hukuchimba, na mashamba ya mizabibu na mizeituni ambayo hukupanda wewe, basi, utakapokula na kushiba,

  19. Kumbukumbu 6:12takriban 1451 KK

    jihadhari usije ukamwacha Bwana, aliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

  20. Kumbukumbu 6:13takriban 1451 KK

    Utamcha Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake.

  21. Kumbukumbu 6:14takriban 1451 KK

    Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka;

  22. Kumbukumbu 6:15takriban 1451 KK

    kwa kuwa Bwana Mungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka uso wa nchi.

  23. Kumbukumbu 6:16takriban 1451 KK

    Usimjaribu Bwana Mungu wako kama ulivyofanya huko Masa.

  24. Kumbukumbu 6:17takriban 1451 KK

    Utayashika maagizo ya Bwana Mungu wako kwa bidii, na masharti na amri alizokupa.

  25. Kumbukumbu 6:18takriban 1451 KK

    Fanya lililo haki na jema mbele za Bwana, ili upate kufanikiwa, uweze kuingia na kuimiliki nchi nzuri ambayo Bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zako,