circa 6 BC – AD 30
The Life of Jesus
The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.
Mistari ya kipindi hiki
- Marko 9:32takriban 32 BK
Lakini wao hawakuelewa kile alimaanisha, nao waliogopa kumuuliza maana yake.
- Marko 9:33takriban 32 BK
Basi wakafika Kapernaumu na baada ya kuingia nyumbani akawauliza, “Mlikuwa mnabishana nini kule njiani?”
- Marko 9:34takriban 32 BK
Lakini hawakumjibu, kwa sababu njiani walikuwa wakibishana kuhusu nani miongoni mwao alikuwa mkuu zaidi ya wote.
- Marko 9:35takriban 32 BK
Akaketi chini, akawaita wote kumi na wawili, akawaambia: “Kama mtu yeyote akitaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa wa mwisho na mtumishi wa wote.”
- Marko 9:36takriban 32 BK
Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao. Akamkumbatia, akawaambia,
- Marko 9:37takriban 32 BK
“Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma.”
- Marko 9:38takriban 32 BK
Yohana akamwambia, “Mwalimu, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamkataza, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”
- Marko 9:39takriban 32 BK
Yesu akasema, “Msimkataze, kwa kuwa hakuna yeyote atendaye miujiza kwa Jina langu ambaye baada ya kitambo kidogo aweza kunena lolote baya dhidi yangu.
- Marko 9:40takriban 32 BK
Kwa maana yeyote asiye kinyume chetu, yuko upande wetu.
- Marko 9:41takriban 32 BK
Amin, nawaambia, yeyote awapaye ninyi kikombe cha maji kwa Jina langu kwa sababu ninyi ni mali ya Kristo, hakika hataikosa thawabu yake.”
- Marko 9:42takriban 32 BK
“Kama mtu yeyote akimsababisha mmojawapo wa wadogo hawa wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa baharini.
- Marko 9:43takriban 32 BK
Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki. [
- Marko 9:44takriban 32 BK
Mahali ambako funza wake hawafi wala moto wake hauzimiki.]
- Marko 9:45takriban 32 BK
Kama mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili lakini ukaingia jehanamu. [
- Marko 9:46takriban 32 BK
Mahali ambako funza wake hawafi wala moto hauzimiki.]
- Marko 9:47takriban 32 BK
Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe. Ni afadhali kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa jehanamu,
- Marko 9:48takriban 32 BK
mahali ambako “ ‘funza wake hawafi, wala moto wake hauzimiki.’
- Marko 9:49takriban 32 BK
Kila mmoja atatiwa chumvi kwa moto.
- Marko 9:50takriban 32 BK
“Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake utaifanyaje ili iweze kukolea tena? Mwe na chumvi ndani yenu, mkaishi kwa amani, kila mmoja na mwenzake.”
- Marko 10:1takriban 29 BK
Yesu akaondoka huko, akavuka Mto Yordani, akaenda sehemu za Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukaenda kwake tena, naye kama ilivyokuwa desturi yake, akawafundisha.
- Marko 10:2takriban 29 BK
Baadhi ya Mafarisayo wakaja ili kumjaribu kwa kumuuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?”
- Marko 10:3takriban 29 BK
Yesu akawajibu, “Je, Mose aliwaamuru nini?”
- Marko 10:4takriban 29 BK
Wakajibu, “Mose aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”
- Marko 10:5takriban 29 BK
Yesu akawaambia, “Mose aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu.
- Marko 10:6takriban 29 BK
Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke.