circa 6 BC – AD 30
The Life of Jesus
The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.
Mistari ya kipindi hiki
- Luka 22:56takriban 33 BK
Mtumishi mmoja wa kike akamwona kwa mwanga wa moto akiwa ameketi pale. Akamtazama sana, akasema, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja na Yesu!”
- Luka 22:57takriban 33 BK
Lakini Petro akakana, akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!”
- Luka 22:58takriban 33 BK
Baadaye kidogo, mtu mwingine alimwona Petro akasema, “Wewe pia ni mmoja wao!” Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sio mmoja wao!”
- Luka 22:59takriban 33 BK
Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akazidi kusisitiza, “Kwa hakika huyu mtu naye alikuwa pamoja na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.”
- Luka 22:60takriban 33 BK
Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!” Wakati huo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika.
- Luka 22:61takriban 33 BK
Naye Bwana akageuka, akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka lile neno ambalo Bwana alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.”
- Luka 22:62takriban 33 BK
Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.
- Luka 22:63takriban 33 BK
Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga.
- Luka 22:64takriban 33 BK
Wakamfunga kitambaa machoni na kumuuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?”
- Luka 22:65takriban 33 BK
Wakaendelea kumtukana kwa matusi mengi.
- Luka 22:66takriban 33 BK
Kulipopambazuka, baraza la wazee wa watu, yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao.
- Luka 22:67takriban 33 BK
Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, tuambie.” Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini.
- Luka 22:68takriban 33 BK
Nami nikiwauliza swali, hamtanijibu.
- Luka 22:69takriban 33 BK
Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.”
- Luka 22:70takriban 33 BK
Wote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?” Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.”
- Luka 22:71takriban 33 BK
Kisha wakasema, “Tuna haja gani tena ya ushahidi zaidi? Tumesikia wenyewe kutoka kinywani mwake.”
- Luka 23:1takriban 33 BK
Kisha umati wote wa watu ukainuka na kumpeleka Yesu kwa Pilato.
- Luka 23:2takriban 33 BK
Nao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.”
- Luka 23:3takriban 33 BK
Basi Pilato akamuuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe wasema.”
- Luka 23:4takriban 33 BK
Pilato akawaambia viongozi wa makuhani na watu wote waliokuwepo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki mtu huyu!”
- Luka 23:5takriban 33 BK
Lakini wao wakakazana kusema, “Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika Uyahudi yote, tangu Galilaya alikoanzia, hadi sehemu hii!”
- Luka 23:6takriban 33 BK
Pilato aliposikia hayo akauliza, “Huyu mtu ni Mgalilaya?”
- Luka 23:7takriban 33 BK
Alipofahamu kwamba Yesu alikuwa chini ya mamlaka ya Herode, akampeleka kwa Herode, ambaye wakati huo alikuwa pia Yerusalemu.
- Luka 23:8takriban 33 BK
Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amesikia mambo mengi kumhusu yeye. Pia alitarajia kumwona akifanya miujiza kadha wa kadha.
- Luka 23:9takriban 33 BK
Herode akamuuliza maswali mengi, lakini Yesu hakumjibu lolote.