Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?” Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.

  2. Siku ile na iwe giza; Mungu juu na asiiangalie; nayo nuru isiiangazie.

  3. Kwa nini uhai hupewa mtu ambaye njia yake imefichika, ambaye Mungu amemzungushia boma?

  4. Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa; kwa mshindo wa hasira zake huangamia.

  5. ‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu? Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake?

  6. Kama Mungu hawaamini watumishi wake, kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea,

  7. “Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, ningeliweka shauri langu mbele zake.

  8. Humwokoa mhitaji kutokana na upanga ulioko kinywani mwao; huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu.

  9. “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.

  10. Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; huumiza, lakini mikono yake pia huponya.

  11. Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga.

  12. Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu, roho yangu inakunywa sumu yake; vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu.

  13. “Laiti ningepata haja yangu, kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia,

  14. kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda, kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali!

  15. Ndipo bado ningekuwa na hii faraja, furaha yangu katika maumivu makali: kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu.

  16. “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake, hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.

  17. Je, mimi ni bahari, au mnyama mkubwa mno akaaye vilindini, hata uniweke chini ya ulinzi?

  18. ndipo wanitisha kwa ndoto na kunitia hofu kwa maono,

  19. “Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki, kwamba unamtia sana maanani,

  20. kwamba unamwangalia kila asubuhi na kumjaribu kila wakati?

  21. Je, hutaacha kamwe kunitazama, au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?

  22. Ikiwa nimetenda dhambi, nimekufanyia nini, Ewe mlinzi wa wanadamu? Kwa nini umeniweka niwe shabaha yako? Je, nimekuwa mzigo kwako?

  23. Kwa nini husamehi makosa yangu na kuachilia dhambi zangu? Kwa kuwa hivi karibuni nitalala mavumbini; nawe utanitafuta, wala sitakuwepo.”

  24. Je, Mungu hupotosha hukumu? Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?

  25. Watoto wako walipomtenda dhambi, aliwapa adhabu ya dhambi yao.