Hesabu 31:27-47
27
Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya.
28
Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili ya Bwana kitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo au mbuzi.
29
Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu ya Bwana.
30
Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya Bwana.”
31
Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Mose.
32
Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000,
33
ngʼombe 72,000,
34
punda 61,000,
35
na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.
36
Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa: Kondoo 337,500
37
ambayo ushuru kwa ajili ya Bwana ilikuwa kondoo 675;
38
ngʼombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa ngʼombe 72;
39
punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa punda 61;
40
Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa watu 32.
41
Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
42
Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Mose aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani,
43
nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500,
44
ngʼombe 36,000,
45
punda 30,500,
46
na wanadamu 16,000.
47
Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama Bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya Bwana.
Settings