Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Waiting Upon God

61 mistari · 68 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. “Ee Bwana, nautafuta wokovu wako.

  2. Alikuwa na wake wawili, mmoja aliitwa Hana na mwingine Penina. Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na mtoto.

  3. Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea atakayeaibishwa, bali wataaibishwa wafanyao hila bila sababu.

  4. niongoze katika kweli yako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.

  5. Uadilifu na uaminifu vinilinde, kwa sababu tumaini langu ni kwako.

  6. Mngojee Bwana, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee Bwana.

  7. Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu.

  8. Tulia mbele za Bwana na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu.

  9. Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.

  10. “Lakini sasa Bwana, nitafute nini? Tumaini langu ni kwako.

  11. Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote, usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu.

  12. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Nilimngoja Bwana kwa saburi, naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

  13. Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda, nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema. Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.

  14. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Wakati Sauli alipotuma wapelelezi nyumbani mwa Daudi ili wamuue. Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu.

  15. Uniponye na watu watendao mabaya, uniokoe kutokana na wamwagao damu.

  16. Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wananifanyia hila, ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea wala kutenda dhambi.

  17. Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia. Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya!

  18. Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli! Zinduka uyaadhibu mataifa yote, usionyeshe huruma kwa wasaliti.

  19. Hurudi wakati wa jioni, wakibweka kama mbwa, wakiuzurura mji.

  20. Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao, hutema upanga kutoka midomo yao, nao husema, “Ni nani atakayetusikia?”

  21. Lakini wewe, Bwana, uwacheke; unayadharau mataifa hayo yote.

  22. Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,

  23. Mungu wangu unipendaye. Mungu atanitangulia, naye atanifanya niwachekelee wale wanaonisingizia.

  24. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko; wokovu wangu watoka kwake.

  25. Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.