Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Strife: General references

124 mistari · 57 vipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. Hivyo Abramu akamwambia Loti, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu.

  2. Akaagana na ndugu zake walipokuwa wakiondoka, akawaambia, “Msigombane njiani!”

  3. Lakini mimi nitawezaje kubeba matatizo yenu, na mizigo yenu, na magomvi yenu peke yangu?

  4. Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako kutokana na hila za wanadamu; katika makao yako huwaweka salama kutokana na ndimi za mashtaka.

  5. Ee Bwana, uwatahayarishe waovu na uwachanganyishie semi zao, maana nimeona jeuri na ugomvi mjini.

  6. Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu, na adui zetu wanatudhihaki.

  7. Usimshtaki mtu bila sababu, wakati hajakutenda dhara lolote.

  8. Mtu mbaya sana na mlaghai, ambaye huzungukazunguka na maneno ya upotovu,

  9. ambaye anakonyeza kwa jicho lake, anayetoa ishara kwa miguu yake na kuashiria kwa vidole vyake,

  10. ambaye hupanga ubaya kwa udanganyifu moyoni mwake: daima huchochea fitina.

  11. Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:

  12. macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia,

  13. moyo uwazao mipango miovu, miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,

  14. shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo, na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.

  15. Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote.

  16. Kiburi huzalisha magomvi tu, bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.

  17. Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.

  18. Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.

  19. Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.

  20. Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji; kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza.

  21. Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; naye ainuaye sana lango lake hutafuta uharibifu.

  22. Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi na kinywa chake hualika kipigo.

  23. Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika kuliko mji uliozungushiwa ngome, nayo mabishano ni kama malango ya ngome yenye makomeo.

  24. Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye, naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.

  25. Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.