Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Strife: Christ, an example of avoiding

12 mistari · 57 vipengele

Mistari kuhusu Christ, an example of avoiding

  1. Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataiinua sauti yake barabarani.

  2. Lakini Yesu alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi wakamfuata, naye akawaponya wagonjwa wao wote,

  3. akiwakataza wasiseme yeye ni nani.

  4. Hii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema:

  5. “Tazama mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Nitaweka Roho wangu juu yake, naye atatangaza haki kwa mataifa.

  6. Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani.

  7. Akatuma watu wamtangulie, nao wakaenda katika kijiji kimoja cha Samaria kumwandalia kila kitu;

  8. lakini watu wa kijiji kile hawakumkaribisha kwa sababu alikuwa anakwenda zake Yerusalemu.

  9. Wanafunzi wake, yaani Yakobo na Yohana, walipoona hayo, wakasema: “Bwana, unataka tuagize moto kutoka mbinguni ili uwaangamize?”

  10. Yesu akageuka na kuwakemea,

  11. nao wakaenda kijiji kingine.

  12. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutishia, bali alijikabidhi kwa yeye ahukumuye kwa haki.