Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Philosophy

90 mistari · 5 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa.

  2. Kama nina hatia, ole wangu! Hata kama ningekuwa sina hatia, siwezi kukiinua kichwa changu, kwa kuwa nimejawa na aibu, na kuzama katika mateso yangu.

  3. Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba, na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu.

  4. Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu na kuzidisha hasira yako juu yangu; nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine.

  5. “Kwa nini basi ulinitoa tumboni? Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona.

  6. Laiti nisingekuwako kamwe, au ningekuwa nimechukuliwa moja kwa moja kutoka tumboni kwenda kaburini!

  7. Je, siku zangu chache si zimekaribia kuisha? Niachie ili niweze kupata muda mfupi wa kufurahi

  8. kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena, katika nchi ya giza na uvuli wa mauti,

  9. Hema za wanyangʼanyi hazisumbuliwi, wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama: wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao.

  10. “Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha, au ndege wa angani, nao watawaambia;

  11. au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha, au acheni samaki wa baharini wawape taarifa.

  12. Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua kwamba mkono wa Bwana ndio uliofanya hili?

  13. Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe, na pumzi ya wanadamu wote.

  14. Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula?

  15. Je, hekima haipatikani katikati ya wazee? Je, maisha marefu hayaleti ufahamu?

  16. “Hekima na nguvu ni vya Mungu; shauri na ufahamu ni vyake yeye.

  17. Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.

  18. Akizuia maji, huwa pana ukame; akiyaachia maji, huharibu nchi.

  19. Kwake kuna nguvu na ushindi; adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake.

  20. Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.

  21. Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme, na kuwafunga mishipi ya kiunoni.

  22. Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.

  23. Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, na kuondoa busara ya wazee.

  24. Huwamwagia dharau wanaoheshimika, na kuwavua silaha wenye nguvu.

  25. Hufunua mambo ya ndani ya gizani, na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana.