Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Jacob: God confirms the covenant of Abraham to

23 mistari · 49 vipengele

Mistari kuhusu God confirms the covenant of Abraham to

  1. Juu yake alisimama Bwana, akasema, “Mimi ni Bwana, Mungu wa baba yako Abrahamu na Mungu wa Isaki. Nchi ambayo umelala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako.

  2. Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi na mashariki, kaskazini na kusini. Kupitia wewe na uzao wako mataifa yote ya duniani yatabarikiwa.

  3. Niko pamoja nawe nami nitakulinda kila uendako na nitakurudisha katika nchi hii. Sitakuacha mpaka nitakapofanya hayo niliyokuahidi.”

  4. Yakobo alipoamka kutoka usingizini, akawaza, “Hakika Bwana yuko mahali hapa, wala mimi sikujua.”

  5. Kwa hiyo akaogopa, akasema, “Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ndipo nyumba ya Mungu ilipo, hili ni lango la mbinguni.”

  6. Asubuhi yake na mapema, Yakobo akalichukua lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.

  7. Mahali pale akapaita Betheli, ingawa mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.

  8. Kisha Yakobo akaweka nadhiri, akisema, “Kama Mungu akiwa pamoja nami na kunilinda katika safari niendayo, akinipa chakula nile na nguo nivae

  9. na nirudi salama nyumbani kwa baba yangu, hapo ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu,

  10. nalo jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu na katika yote utakayonipa nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”

  11. Baada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki.

  12. Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini hutaitwa tena Yakobo, jina lako utakuwa Israeli.” Kwa hiyo akamwita Israeli.

  13. Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi, ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako.

  14. Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.”

  15. Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye.

  16. Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake.

  17. Yakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Betheli.

  18. enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

  19. Yeye ndiye Bwana Mungu wetu; hukumu zake zimo duniani pote.

  20. Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,

  21. agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki.

  22. Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele:

  23. “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.”