Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 21:15takriban 1453 KK

    na miteremko ya mabonde inayofika hadi mji wa Ari na huelekea mpakani mwa Moabu.”

  2. Hesabu 21:16takriban 1453 KK

    Kutoka hapo waliendelea mbele hadi kisima cha Beeri; kwenye kisima ambacho Bwana alimwambia Mose, “Wakusanye watu pamoja, nami nitawapa maji.”

  3. Hesabu 21:17takriban 1453 KK

    Kisha Israeli akaimba wimbo huu: “Bubujika, ee kisima! Imba kuhusu maji,

  4. Hesabu 21:18takriban 1453 KK

    kuhusu kisima ambacho kilichimbwa na wakuu, ambacho watu mashuhuri walikifukua, watu mashuhuri wakiwa na fimbo za utawala na bakora.” Kisha wakatoka jangwani kwenda Matana,

  5. Hesabu 21:19takriban 1453 KK

    kutoka Matana wakafika Nahalieli, kutoka Nahalieli wakafika Bamothi,

  6. Hesabu 21:20takriban 1453 KK

    na kutoka Bamothi wakafika kwenye bonde lililoko Moabu, mahali ambapo kilele cha Pisga kinatazamana na nyika.

  7. Hesabu 21:21takriban 1453 KK

    Israeli akawatuma wajumbe kumwambia Sihoni mfalme wa Waamori:

  8. Hesabu 21:22takriban 1453 KK

    “Uturuhusu tupite katika nchi yako. Hatutageuka kando kwenda katika mashamba au mashamba ya mizabibu, ama kunywa maji kutoka kisima chochote. Tutasafiri kwenye njia kuu ya mfalme hata tutakapokuwa tumekwisha kupita katika nchi yako.”

  9. Hesabu 21:23takriban 1453 KK

    Lakini Sihoni hakumruhusu Israeli apite katika nchi yake. Alilikutanisha jeshi lake lote, wakaondoka kwenda jangwani ili kupigana na Israeli. Alipofika huko Yahazi, akapigana na Israeli.

  10. Hesabu 21:24takriban 1453 KK

    Hata hivyo, Israeli alimshinda kwa upanga na kuiteka ardhi yake kutoka Arnoni mpaka Yaboki, lakini ni hadi kufikia nchi ya Waamoni tu, kwa sababu mipaka yake ilikuwa imezungushwa ukuta.

  11. Hesabu 21:25takriban 1453 KK

    Israeli akaiteka miji yote ya Waamori na kuikalia, pamoja na Heshboni na makazi yote yanayoizunguka.

  12. Hesabu 21:26takriban 1453 KK

    Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa amepigana dhidi ya mfalme wa Moabu aliyetangulia na akawa amechukua ardhi yake yote mpaka Arnoni.

  13. Hesabu 21:27takriban 1453 KK

    Ndiyo sababu watunga mashairi husema: “Njoo Heshboni na ujengwe tena; mji wa Sihoni na ufanywe upya.

  14. Hesabu 21:28takriban 1453 KK

    “Moto uliwaka kutoka Heshboni, mwali wa moto kutoka mji wa Sihoni. Uliteketeza Ari ya Moabu, raiya wa mahali pa Arnoni palipoinuka.

  15. Hesabu 21:29takriban 1453 KK

    Ole wako, ee Moabu! Umeharibiwa, enyi watu wa Kemoshi! Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi, na binti zake kama mateka kwa Mfalme Sihoni wa Waamori.

  16. Hesabu 21:30takriban 1453 KK

    “Lakini tumewashinda; Heshboni umeharibiwa hadi Diboni. Tumebomoa hadi kufikia Nofa, ulioenea hadi Medeba.”

  17. Hesabu 21:31takriban 1453 KK

    Kwa hiyo Israeli akaishi katika nchi ya Waamori.

  18. Hesabu 21:32takriban 1453 KK

    Baada ya Mose kutuma wapelelezi kwenda mji wa Yazeri, Waisraeli waliteka viunga vya mji huo na kuwafukuza Waamori waliokuwa wanaishi huko.

  19. Hesabu 21:33takriban 1453 KK

    Kisha wakageuka na kwenda katika njia inayoelekea Bashani, naye Ogu mfalme wa Bashani pamoja na jeshi lake lote wakatoka kupigana nao huko Edrei.

  20. Hesabu 21:34takriban 1453 KK

    Bwana akamwambia Mose, “Usimwogope Ogu, kwa sababu nimeshamkabidhi mikononi mwako, pamoja na jeshi lake lote na nchi yake. Mtendee kama ulivyomtendea Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.”

  21. Hesabu 21:35takriban 1453 KK

    Kwa hiyo wakamuua, pamoja na wanawe na jeshi lake lote, bila ya kumwacha hata mtu mmoja hai. Nao wakaimiliki nchi yake.

  22. Hesabu 22:1takriban 1452 KK

    Kisha Waisraeli wakasafiri katika tambarare za Moabu na kupiga kambi kando ya Mto Yordani, ngʼambo ya Yeriko.

  23. Hesabu 22:2takriban 1452 KK

    Basi Balaki mwana wa Sipori, aliona mambo yale yote ambayo Israeli aliwatendea Waamori,

  24. Hesabu 22:3takriban 1452 KK

    Moabu aliogopa, kwa kuwa walikuwepo watu wengi sana. Hakika, Moabu alijawa na hofu kubwa kwa sababu ya Waisraeli.

  25. Hesabu 22:4takriban 1452 KK

    Wamoabu wakawaambia wazee wa Midiani, “Umati huu wa watu unakwenda kuramba kila kitu kinachotuzunguka, kama maksai arambavyo majani ya shambani.” Kwa hiyo Balaki mwana wa Sipori, ambaye alikuwa mfalme wa Moabu wakati huo,