Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 27:16takriban 33 BK

    Wakati huo alikuwepo mfungwa mmoja mwenye sifa mbaya, aliyeitwa Baraba.

  2. Mathayo 27:17takriban 33 BK

    Hivyo umati wa watu walipokusanyika, Pilato akawauliza, “Mnataka niwafungulie nani, Baraba au Yesu yeye aitwaye Kristo?”

  3. Mathayo 27:18takriban 33 BK

    Kwa kuwa alitambua Yesu alikuwa amekabidhiwa kwake kwa ajili ya wivu.

  4. Mathayo 27:19takriban 33 BK

    Pilato akiwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akampelekea ujumbe huu: “Usiwe na jambo lolote juu ya mtu huyu asiye na hatia, kwa kuwa leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake.”

  5. Mathayo 27:20takriban 33 BK

    Lakini viongozi wa makuhani na wazee wakaushawishi ule umati wa watu kwamba waombe Baraba afunguliwe, naye Yesu auawe.

  6. Mathayo 27:21takriban 33 BK

    Mtawala akawauliza tena, “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka niwafungulie?” Wakajibu, “Baraba.”

  7. Mathayo 27:22takriban 33 BK

    Pilato akawaambia, “Basi nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?” Wakajibu wote, “Msulubishe!”

  8. Mathayo 27:23takriban 33 BK

    Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupiga kelele, wakisema, “Msulubishe!”

  9. Mathayo 27:24takriban 33 BK

    Pilato alipoona kwamba hawezi kufanya lolote, lakini badala yake ghasia zilikuwa zinaanza, akachukua maji, akanawa mikono yake mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Sina hatia juu ya damu ya mtu huyu, hili ni jukumu lenu!”

  10. Mathayo 27:25takriban 33 BK

    Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”

  11. Mathayo 27:26takriban 33 BK

    Basi akawafungulia Baraba. Lakini baada ya kuamuru Yesu achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe.

  12. Mathayo 27:27takriban 33 BK

    Kisha askari wa mtawala wakampeleka Yesu kwenye Praitorio na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka.

  13. Mathayo 27:28takriban 33 BK

    Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha

  14. Mathayo 27:29takriban 33 BK

    wakasokota taji ya miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!”

  15. Mathayo 27:30takriban 33 BK

    Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena.

  16. Mathayo 27:31takriban 33 BK

    Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili wakamsulubishe.

  17. Mathayo 27:32takriban 33 BK

    Walipokuwa wakienda, wakakutana na mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba.

  18. Mathayo 27:33takriban 33 BK

    Wakafika mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa).

  19. Mathayo 27:34takriban 33 BK

    Hapo wakampa Yesu divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini alipoionja, akakataa kuinywa.

  20. Mathayo 27:35takriban 33 BK

    Walipokwisha kumsulubisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura. [Hili lilifanyika ili litimie lile neno lililonenwa na nabii, “Waligawa nguo zangu miongoni mwao na vazi langu wakalipigia kura.”]

  21. Mathayo 27:36takriban 33 BK

    Kisha wakaketi, wakamchunga.

  22. Mathayo 27:37takriban 33 BK

    Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake hivi: Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi.

  23. Mathayo 27:38takriban 33 BK

    Wanyangʼanyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wa kushoto.

  24. Mathayo 27:39takriban 33 BK

    Watu waliokuwa wakipita njiani wakamtukana huku wakitikisa vichwa vyao

  25. Mathayo 27:40takriban 33 BK

    na kusema, “Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe mwenyewe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu, shuka kutoka msalabani.”