Rukia maudhui

circa AD 30–62

The Early Church

Pentecost ignites a movement; Peter, Paul, and countless others carry the gospel from Jerusalem to the ends of the earth.

1,007 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Matendo 27:19takriban 62 BK

    Siku ya tatu, wakatupa vyombo vya meli baharini kwa mikono yao wenyewe.

  2. Matendo 27:20takriban 62 BK

    Kulipokuwa hakuna kuonekana kwa jua wala nyota kwa siku nyingi, nayo dhoruba ikiwa inaendelea kuwa kali, hatimaye tulikata kabisa tamaa ya kuokoka.

  3. Matendo 27:21takriban 62 BK

    Baada ya watu kukaa siku nyingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati yao akasema, “Enyi watu, iliwapasa kunisikiliza na kuacha kusafiri baharini kutoka Krete, ndipo ninyi mngekuwa mmejinusuru na uharibifu huu na hasara hii.

  4. Matendo 27:22takriban 62 BK

    Sasa ninawasihi sana, jipeni moyo mkuu kwa kuwa hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake, ila meli itaangamia.

  5. Matendo 27:23takriban 62 BK

    Jana usiku, malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake na ambaye ninamwabudu alisimama karibu nami,

  6. Matendo 27:24takriban 62 BK

    naye akasema, ‘Paulo usiogope, kwa kuwa ni lazima usimame mbele ya Kaisari, naye Mungu amekupa kwa neema uhai wa wote wanaosafiri pamoja nawe.

  7. Matendo 27:25takriban 62 BK

    Hivyo jipeni moyo, enyi watu, kwa kuwa ninamwamini Mungu kwamba yatakuwa kama vile alivyoniambia.’

  8. Matendo 27:26takriban 62 BK

    Lakini hata hivyo meli yetu itakwama kwenye kisiwa fulani.”

  9. Matendo 27:27takriban 62 BK

    Usiku wa kumi na nne ulipofika, tulikuwa bado tunasukumwa na upepo katika Bahari ya Adria. Ilipokuwa yapata usiku wa manane, mabaharia wakahisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu.

  10. Matendo 27:28takriban 62 BK

    Kwa hiyo wakapima kina cha maji na kukuta kilikuwa pima ishirini, baada ya kuendelea mbele kidogo wakapima tena wakapata kina cha pima kumi na tano.

  11. Matendo 27:29takriban 62 BK

    Wakiogopa kwamba meli yetu ingegonga kwenye miamba, wakashusha nanga nne za nyuma ya meli, wakawa wanaomba kupambazuke.

  12. Matendo 27:30takriban 62 BK

    Katika jaribio la kutoroka kutoka kwenye meli, mabaharia wakashusha mashua ya kuokolea watu baharini, wakijifanya kwamba wanakwenda kushusha nanga za omo.

  13. Matendo 27:31takriban 62 BK

    Ndipo Paulo akamwambia yule jemadari na askari, “Hawa watu wasipobaki katika meli, hamtaweza kuokoka.”

  14. Matendo 27:32takriban 62 BK

    Hivyo basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua ya kuokolea watu kwenye meli, wakaiacha ianguke humo baharini.

  15. Matendo 27:33takriban 62 BK

    Kabla ya mapambazuko, Paulo akawasihi watu wote wale chakula akisema, “Leo ni siku ya kumi na nne mmekuwa katika wasiwasi mkiwa mmefunga na bila kula chochote.

  16. Matendo 27:34takriban 62 BK

    Kwa hiyo nawasihi mle chakula, kwa maana itawasaidia ili mweze kuishi. Kwa kuwa hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza unywele hata mmoja kutoka kichwani mwake.”

  17. Matendo 27:35takriban 62 BK

    Baada ya kusema maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula.

  18. Matendo 27:36takriban 62 BK

    Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chakula.

  19. Matendo 27:37takriban 62 BK

    Ndani ya meli tulikuwa jumla ya watu 276.

  20. Matendo 27:38takriban 62 BK

    Baada ya watu wote kula chakula cha kutosha, wakapunguza uzito wa meli kwa kutupa ngano baharini.

  21. Matendo 27:39takriban 62 BK

    Kulipopambazuka, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga, ambako waliamua kuipweleza meli kama ingewezekana.

  22. Matendo 27:40takriban 62 BK

    Kwa hiyo wakatupa nanga zote na kuziacha baharini, na wakati huo huo wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli. Kisha wakatweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani.

  23. Matendo 27:41takriban 62 BK

    Lakini wakafika mahali ambapo bahari mbili zinakutana, wakaipweleza meli ufuoni, omo ikakwama sana, ikawa haiwezi kuondolewa, lakini sehemu ya shetri ikavunjika vipande vipande kwa kule kupiga kwa mawimbi yenye nguvu.

  24. Matendo 27:42takriban 62 BK

    Wale askari wakapanga kuwaua wale wafungwa ili kuzuia hata mmoja wao asiogelee na kutoroka.

  25. Matendo 27:43takriban 62 BK

    Lakini yule jemadari alitaka kuokoa maisha ya Paulo, basi akawazuia askari wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, waogelee mpaka nchi kavu.