Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Walawi 23:21takriban 1490 KK

    Siku iyo hiyo mtatangaza kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi.

  2. Walawi 23:22takriban 1490 KK

    “ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu, au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

  3. Walawi 23:23takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  4. Walawi 23:24takriban 1490 KK

    “Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na siku ya mapumziko, kusanyiko takatifu la ukumbusho litakaloadhimishwa kwa kupiga tarumbeta.

  5. Walawi 23:25takriban 1490 KK

    Msifanye kazi zenu zozote za kawaida, lakini toeni sadaka kwa Bwana iliyoteketezwa kwa moto.’ ”

  6. Walawi 23:26takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  7. Walawi 23:27takriban 1490 KK

    “Siku ya kumi ya mwezi huu wa saba ni Siku ya Upatanisho. Mtafanya kusanyiko takatifu, mfunge, nanyi mtoe sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto.

  8. Walawi 23:28takriban 1490 KK

    Msifanye kazi siku hiyo, kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, ambapo upatanisho unafanyika kwa ajili yenu mbele za Bwana Mungu wenu.

  9. Walawi 23:29takriban 1490 KK

    Mtu yeyote ambaye hatafunga siku hiyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

  10. Walawi 23:30takriban 1490 KK

    Mtu yeyote atakayefanya kazi siku hiyo nitamwangamiza kutoka miongoni mwa watu wake.

  11. Walawi 23:31takriban 1490 KK

    Hamtafanya kazi kamwe. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo popote mnapoishi.

  12. Walawi 23:32takriban 1490 KK

    Ni Sabato ya mapumziko kwenu ninyi, na lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.”

  13. Walawi 23:33takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  14. Walawi 23:34takriban 1490 KK

    “Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, Sikukuu ya Bwana ya vibanda itaanza, nayo itaadhimishwa kwa siku saba.

  15. Walawi 23:35takriban 1490 KK

    Siku ya kwanza ni kusanyiko takatifu, msifanye kazi zenu za kawaida.

  16. Walawi 23:36takriban 1490 KK

    Kwa siku saba toeni sadaka kwa Bwana za kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na mtoe sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.

  17. Walawi 23:37takriban 1490 KK

    (“ ‘Hizi ni sikukuu za Bwana zilizoamriwa, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu kwa kuleta sadaka kwa Bwana za kuteketeza kwa moto: sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, dhabihu na sadaka za vinywaji zitahitajika kila siku.

  18. Walawi 23:38takriban 1490 KK

    Sadaka hizi ni nyongeza ya zile mnazozitoa katika Sabato za Bwana, na pia ni nyongeza ya matoleo yenu ya chochote mlichoweka nadhiri, na sadaka zenu zote za hiari mnazozitoa kwa Bwana.)

  19. Walawi 23:39takriban 1490 KK

    “ ‘Basi kuanzia siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, baada ya kuvuna mazao yote ya nchi, mtaadhimisha sikukuu kwa Bwana kwa siku saba; siku ya kwanza ni mapumziko, pia siku ya nane ni mapumziko.

  20. Walawi 23:40takriban 1490 KK

    Siku ya kwanza mtachukua matunda mazuri ya miti, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi, na matawi ya mirebi, nanyi mtashangilia mbele za Bwana Mungu wenu kwa siku saba.

  21. Walawi 23:41takriban 1490 KK

    Mtaadhimisha siku hii kuwa sikukuu kwa Bwana kwa siku saba kila mwaka. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo; iadhimisheni mwezi wa saba.

  22. Walawi 23:42takriban 1490 KK

    Mtaishi katika vibanda kwa siku saba: Wazawa wote wa Waisraeli wataishi katika vibanda,

  23. Walawi 23:43takriban 1490 KK

    ili wazao wenu wajue kuwa niliwafanya Waisraeli waishi kwenye vibanda nilipowatoa Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

  24. Walawi 23:44takriban 1490 KK

    Kwa hiyo Mose akawatangazia Waisraeli sikukuu zilizoamriwa na Bwana.

  25. Walawi 24:1takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,