Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Walawi 24:2takriban 1490 KK

    “Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima.

  2. Walawi 24:3takriban 1490 KK

    Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.

  3. Walawi 24:4takriban 1490 KK

    Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima.

  4. Walawi 24:5takriban 1490 KK

    “Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa za unga kwa kila mkate.

  5. Walawi 24:6takriban 1490 KK

    Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za Bwana juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi.

  6. Walawi 24:7takriban 1490 KK

    Kando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto.

  7. Walawi 24:8takriban 1490 KK

    Mikate hii itawekwa mbele za Bwana kila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa Agano la kudumu.

  8. Walawi 24:9takriban 1490 KK

    Hii ni mali ya Aroni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto.”

  9. Walawi 24:10takriban 1490 KK

    Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli.

  10. Walawi 24:11takriban 1490 KK

    Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina la Bwana kwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri, wa kabila la Dani.)

  11. Walawi 24:12takriban 1490 KK

    Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi ya Bwana yawe wazi kwao.

  12. Walawi 24:13takriban 1490 KK

    Ndipo Bwana akamwambia Mose:

  13. Walawi 24:14takriban 1490 KK

    “Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe.

  14. Walawi 24:15takriban 1490 KK

    Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake;

  15. Walawi 24:16takriban 1490 KK

    yeyote atakayekufuru Jina la Bwana ni lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwe ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la Bwana, ni lazima auawe.

  16. Walawi 24:17takriban 1490 KK

    “ ‘Kama mtu yeyote atamuua mtu mwingine, ni lazima auawe.

  17. Walawi 24:18takriban 1490 KK

    Mtu yeyote auaye mnyama wa mtu mwingine lazima afidie, uhai kwa uhai.

  18. Walawi 24:19takriban 1490 KK

    Ikiwa mtu yeyote atamjeruhi jirani yake, chochote alichomtenda naye atatendewa:

  19. Walawi 24:20takriban 1490 KK

    iwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa.

  20. Walawi 24:21takriban 1490 KK

    Yeyote auaye mnyama wa mtu lazima alipe fidia, lakini yeyote auaye mtu, lazima auawe.

  21. Walawi 24:22takriban 1490 KK

    Mtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

  22. Walawi 24:23takriban 1490 KK

    Kisha Mose akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Mose.

  23. Walawi 25:1takriban 1491 KK

    Bwana akamwambia Mose katika Mlima Sinai,

  24. Walawi 25:2takriban 1491 KK

    “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapa ninyi, nchi yenyewe ni lazima ishike Sabato kwa ajili ya Bwana.

  25. Walawi 25:3takriban 1491 KK

    Kwa miaka sita mtapanda mazao katika mashamba yenu, nanyi kwa miaka sita mtaikata mizabibu yenu matawi na kuvuna mazao yake.