Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani.

  2. Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha.

  3. Kambini walimwonea wivu Mose, na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana.

  4. Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri,

  5. Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza: kama Mose mteule wake, asingesimama kati yao na Mungu kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza.

  6. Kisha waliidharau ile nchi nzuri, hawakuiamini ahadi yake.

  7. Walinungʼunika ndani ya mahema yao, wala hawakumtii Bwana.

  8. Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba atawafanya waanguke jangwani,

  9. Waliichochea hasira ya Bwana, wakamkasirisha kwa matendo yao maovu, nayo tauni ikazuka katikati yao.

  10. Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana, janga likampata Mose kwa sababu yao;

  11. Hawakuyaangamiza yale mataifa kama Bwana alivyowaagiza,

  12. Kwa hiyo Bwana akawakasirikia watu wake na akauchukia sana urithi wake.

  13. Akawakabidhi kwa mataifa na adui zao wakawatawala.

  14. Mara nyingi aliwaokoa lakini walikuwa wamezama kwenye uasi, nao wakajiharibu katika dhambi zao.

  15. Lakini akaangalia mateso yao wakati aliposikia kilio chao;

  16. kwa ajili yao akakumbuka agano lake, na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake.

  17. Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe. Tukusanye tena kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kushangilia katika sifa zako.

  18. Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Watu wote na waseme, “Amen!” Msifuni Bwana.

  19. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele.

  20. Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi, wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui,

  21. Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.

  22. Akawaongoza kwa njia iliyo sawa hadi mji ambao wangeweza kuishi.

  23. Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,

  24. kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu, na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema.

  25. kwa sababu walikuwa wameasi dhidi ya maneno ya Mungu na kudharau shauri la Aliye Juu Sana.