Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu.

  2. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, ambaye ninakusifu, usiwe kimya,

  3. Agiza mtu mwovu ampinge, mshtaki asimame mkono wake wa kuume.

  4. Maovu ya baba zake na yakumbukwe mbele za Bwana, dhambi ya mama yake isifutwe kamwe.

  5. Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana, ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani.

  6. Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu, kwa wale wanaoninenea mabaya.

  7. Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi, unitendee wema kwa ajili ya jina lako, uniokoe kwa wema wa pendo lako.

  8. Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie, niokoe sawasawa na upendo wako.

  9. Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili.

  10. Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki, watakaposhambulia wataaibishwa, lakini mtumishi wako atashangilia.

  11. Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana, katika umati mkubwa nitamsifu.

  12. Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji, kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu.

  13. Zaburi ya Daudi. Bwana amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”

  14. Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; utatawala katikati ya adui zako.

  15. Askari wako watajitolea kwa hiari katika siku yako ya vita. Ukiwa umevikwa fahari takatifu, kutoka tumbo la mapambazuko utapokea umande wa ujana wako.

  16. Bwana ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.”

  17. Bwana yuko mkono wako wa kuume, atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.

  18. Msifuni Bwana. Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.

  19. Kazi za Bwana ni kuu, wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.

  20. Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima.

  21. Amefanya maajabu yake yakumbukwe, Bwana ni mwenye neema na huruma.

  22. Huwapa chakula wale wanaomcha, hulikumbuka agano lake milele.

  23. Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine.

  24. Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, mausia yake yote ni ya kuaminika.

  25. Aliwapa watu wake ukombozi, aliamuru agano lake milele: jina lake ni takatifu na la kuogopwa.