Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia.

  2. Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.

  3. Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,

  4. kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba na kukata mapingo ya chuma.

  5. Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.

  6. Akalituma neno lake na kuwaponya, akawaokoa kutoka maangamizo yao.

  7. Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

  8. Na watoe dhabihu za kushukuru, na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha.

  9. Waliziona kazi za Bwana, matendo yake ya ajabu kilindini.

  10. Kwa maana alisema na kuamsha tufani iliyoinua mawimbi juu.

  11. Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawatoa kwenye taabu yao.

  12. Walifurahi ilipokuwa shwari, naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani.

  13. Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

  14. Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee.

  15. aliwaleta wenye njaa wakaishi humo, nao wakajenga mji wangeweza kuishi.

  16. Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao, na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo.

  17. Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya, na atafakari upendo mkuu wa Bwana.

  18. Wimbo. Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

  19. Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.

  20. Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu; uaminifu wako unazifikia anga.

  21. Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote.

  22. Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa.

  23. Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi.

  24. Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”

  25. Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu?