Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki.

  2. “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.”

  3. Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:

  4. “Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.”

  5. Akaiita njaa juu ya nchi na kuharibu chakula chao chote,

  6. hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia, hadi neno la Bwana lilipomthibitisha.

  7. Bwana aliwafanya watu wake kuzaana sana, akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao,

  8. ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake, wakatenda hila dhidi ya watumishi wake.

  9. Akamtuma Mose mtumishi wake, pamoja na Aroni, aliyemchagua.

  10. Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao, miujiza yake katika nchi ya Hamu.

  11. Alituma giza na nchi ikajaa giza, kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?

  12. Waliomba, naye akawaletea kware, akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.

  13. Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake.

  14. Aliwatoa watu wake kwa furaha, wateule wake kwa kelele za shangwe,

  15. alifanya haya ili wayashike mausia yake na kuzitii sheria zake. Msifuni Bwana.

  16. Msifuni Bwana. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

  17. Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana au kutangaza kikamilifu sifa zake?

  18. Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, uwe msaada wangu unapowaokoa,

  19. ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako, niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako, na kuungana na urithi wako katika kukusifu.

  20. Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.

  21. Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake, ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu.

  22. Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.

  23. Aliwaokoa mikononi mwa adui; kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa.

  24. Ndipo walipoamini ahadi zake, nao wakaimba sifa zake.

  25. Lakini mara walisahau aliyowatendea, wala hawakungojea shauri lake.