Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele.

  2. Msifuni Bwana. Heri mtu yule amchaye Bwana, mtu yule apendezwaye sana na amri zake.

  3. Hataogopa habari mbaya, moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.

  4. Msifuni Bwana. Enyi watumishi wa Bwana msifuni, lisifuni jina la Bwana.

  5. Jina la Bwana na lisifiwe, sasa na hata milele.

  6. Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Bwana linapaswa kusifiwa.

  7. Bwana ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu.

  8. Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu, Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi,

  9. ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi?

  10. huwaketisha pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake.

  11. Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake, akiwa mama watoto mwenye furaha. Msifuni Bwana.

  12. Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, Israeli akawa milki yake.

  13. Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo,

  14. Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi, bali utukufu ni kwa jina lako, kwa sababu ya upendo na uaminifu wako.

  15. Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wao?”

  16. Mungu wetu yuko mbinguni, naye hufanya lolote limpendezalo.

  17. Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.

  18. Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.

  19. Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.

  20. Bwana anatukumbuka na atatubariki: ataibariki nyumba ya Israeli, ataibariki nyumba ya Aroni,

  21. atawabariki wale wanaomcha Bwana, wadogo kwa wakubwa.

  22. Bwana na awawezeshe kuongezeka, ninyi na watoto wenu.

  23. Mbarikiwe na Bwana Muumba wa mbingu na dunia.

  24. Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana, lakini dunia amempa mwanadamu.

  25. Sio wafu wanaomsifu Bwana, wale washukao mahali pa kimya,