God
Mistari inayomtaja God
bali ni sisi tunaomtukuza Bwana, sasa na hata milele. Msifuni Bwana.
Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie.
Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu.
Ndipo nikaliitia jina la Bwana: “Ee Bwana, niokoe!”
Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma.
Bwana huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.
Ee nafsi yangu, tulia tena, kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako.
Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umeniokoa nafsi yangu na mauti, macho yangu kutokana na machozi, miguu yangu kutokana na kujikwaa,
ili niweze kutembea mbele za Bwana, katika nchi ya walio hai.
Nimrudishie Bwana nini kwa wema wake wote alionitendea?
Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la Bwana.
Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote.
Kifo cha watakatifu kina thamani machoni pa Bwana.
Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umeniweka huru toka katika minyororo yangu.
Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la Bwana.
Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote,
katika nyua za nyumba ya Bwana, katikati yako, ee Yerusalemu. Msifuni Bwana.
Msifuni Bwana, enyi mataifa yote; mtukuzeni yeye, enyi watu wote.
Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu, uaminifu wa Bwana unadumu milele. Msifuni Bwana.
Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.
Israeli na aseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
Wote wamchao Bwana na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”
Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana, naye akanijibu kwa kuniweka huru.
Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?